top of page

Furaha Isiyozuilika

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 30
  • 2 min read
ree

“Nimefanya Jina lako lijulikane kwao, nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao, na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao” (Yohana 17:26)


Hivyo ndivyo Yesu aliomba usiku kabla ya kufa kwake. Fikiria kuwa na uwezo wa kufurahia kile kinachofurahisha zaidi kwa nguvu na shauku isiyo na mipaka milele. Huu sio uzoefu wetu wa sasa. Mambo matatu yanazuia utoshelevu wetu kamili katika ulimwengu huu.


  • Moja ni kwamba hakuna kitu katika ulimwengu huu ulioumbwa chenye thamani ya kibinafsi ya kutosha kukidhi tamaa za kina za mioyo yetu.


  • Nyingine ni kwamba tunakosa nguvu ya kufurahia hazina bora kwa thamani yake ya juu kabisa.


  • Na kikwazo cha tatu kinachozuia kuridhika kikamilifu ni kwamba furaha zetu hapa zinafikia kikomo. Hakuna kinachodumu. Lakini ikiwa lengo na maombi ya Yesu katika Yohana 17:26 yatatimia, haya yote yatabadilika. Alisali “ili pendo ambalo wewe, Baba, umenipenda nalo, liwe ndani yao.” Upendo wa Mungu usio na kifani kwa Mwana Wake ndani yetu!


Ikiwa furaha ya Mungu kwa Mwana inakuwa furaha yetu kwa Mwana, basi lengo la furaha yetu, Yesu, litakuwa na thamani isiyokoma ya kibinafsi. Hatawahi kutuchosha au kutusikitisha au kutukatisha tamaa.


Hakuna hazina kubwa zaidi inayoweza kupatikana kuliko Mwana wa Mungu.


Zaidi ya hayo, uwezo wetu wa kufurahia hazina hiyo isiyoisha hautazuiliwa na udhaifu wa kibinadamu. Tutamfurahia Mwana wa Mungu kwa furaha ile ile ya Baba yake. Hicho ndicho Yesu alichokimbea!


Furaha ya Mungu katika Mwana wake itakuwa ndani yetu na itakuwa yetu - furaha yetu katika Mwana. Na hili halitaisha, kwa sababu Baba wala Mwana hawana mwisho.

Upendo wao kwa kila mmoja wao utakuwa upendo wetu kwao na kwa hivyo upendo wetu kwao hautakufa kamwe, wala kupungua.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page