top of page

Kitu Chenye Kutosheleza Yote

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 30
  • 1 min read
ree

Jifurahishe katika Bwana, naye atakupa haja za moyo wako. (Zaburi 37:4)

 

Kule kutafuta furaha si kitu cha hiari tu, bali ni amri (katika Zaburi): "Jifurahishe kwa Bwana, naye atakupa haja za moyo wako" (Zaburi 37:4).

 

Watunga-zaburi walitaka kufanya hivi: “Kama paa anavyo onea shauku vijito vya maji vinavyo tiririka, ndivyo nafsi yangu inavyo kuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu ina kiu ya Mungu, Mungu aliye hai” (Zaburi 42:1–2). “Nafsi yangu ina kiu kwa ajili yako; mwili wangu una zimia kwa ajili yako, kama katika nchi kavu na uchovu, isiyo na maji” (Zaburi 63:1).

 

Nia ya kuwa na kiu ina ulinganifu wake wenye kuridhisha wakati mtunga-zaburi asemapo kwamba watu “wanywe na kushiba wingi wa nyumba yako; nawe ukawa nywesha mto wa furaha zako” (Zaburi 36:8).

 

Niligundua kwamba wema wa Mungu, msingi wa ibada, si kitu unachokiheshimu kwa aina fulani ya heshima isiyo na shauku. La, ni jambo la kufurahia: “Onjeni mwone ya kuwa Bwana ni mwema!” (Zaburi 34:8). Onja. Onja! Na uone.

 

Maneno yako ni matamu kama nini kwangu, Ni matamu kuliko asali kinywani mwangu!

 

Kama CS Lewis asemavyo, Mungu katika Zaburi ndiye "Mwenye kutosheleza” Watu wake wanamwabudu bila haya kwa ajili ya "furaha kuu" wanayopata ndani yake (Zaburi 43:4). Yeye ndiye chanzo cha furaha kamili na isiyo na mwisho: “Mbele za uwepo wako mna furaha tele; mkono wako wa kuume kuna mema ya milele” (Zaburi 16:11).

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page