top of page

Yesu Anawajua Kondoo Wake

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 2 min read

Updated: May 1

ree

“Kondoo wangu huisikia sauti yangu, nami nawajua.” (Yohana 10:27)


Yesu anawajua walio wake. Maarifa gani haya?

 

Yohana 10:3 ni ulinganifu wa karibu na Yohana 10:27. Inasema, "Kondoo huisikia sauti yake, naye huwaita kondoo wake kwa majina na kuwaongoza nje."

 

Kwa hiyo, Yesu anaposema, “Nawajua,” hii ina maana angalau kwamba anawajua kwa majina; yaani anawajua mmoja mmoja na kwa ukaribu. Sio kwamba hawajajulikana, wamepotea na kuchanganyika kwenye kundi.

 

Yohana 10:14–15 inatoa utambuzi mwingine: “Mimi ndimi mchungaji mwema. Nawajua walio wangu na walio wangu wananijua mimi, kama vile Baba anijuavyo nami ninamjua Baba.”

 

Kuna mfanano wa kweli kati ya jinsi Yesu anavyomjua Baba yake wa mbinguni na jinsi anavyowajua kondoo wake. Yesu anajiona ndani ya Baba, na anajiona ndani ya wanafunzi wake.

 

Kujulikana kibinafsi, kwa ukaribu, na kwa upendo na Mwana wa Mungu ni upendeleo mkubwa na zawadi ya thamani, ikijumuisha ushirika binafsi na ahadi ya uzima wa milele.

Kwa kiasi fulani Yesu anatambua tabia yake mwenyewe ndani ya wanafunzi wake. Anaona chapa yake mwenyewe kwa kondoo. Hii inawafanya wapendezwe naye.

 

Yeye ni kama mume anayemngoja mke wake kwenye uwanja wa ndege, akitazama kila mtu akishuka kutoka kwenye ndege. Anapoonekana, anamjua, anatambua sifa zake, anaona machoni pake onyesho la furaha la upendo wake mwenyewe. Anapendezwa nae. Yeye pekee ndiye anayemkumbatia.

 

Mtume Paulo anaiweka hivi: Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, ukiwa na muhuri wenye maandishi haya: “Bwana anawajua walio wake” (2 Timotheo 2:19).

 

Ni vigumu kukazia zaidi sana jinsi ulivyo upendeleo mkubwa kujulikana kibinafsi, kwa ukaribu, na kwa upendo na Mwana wa Mungu. Ni zawadi ya thamani kwa kondoo wake wote, na ndani yake ina ushirika binafsi, na shauku na ahadi ya uzima wa milele.



Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page