JE, UNAJISIKIAJE KUHUSU MAFUNDISHO YA IMANI?
Haijalishi jibu lako ni nini, kitabu hiki hakitakushawishi tu kwamba mafundisho sahihi ni muhimu kwenye kuishi maisha ya kumcha Mungu, bali pia kitaeleza nafasi ya msingi ya theolojia katika maisha ya kanisa lenye afya njema. Mwishowe, kufikiri vyema kuhusu Mungu kunaathiri kila kitu—kuanzia kutuongoza katika masuala ya kiutendaji hadi kukuza umoja na ushuhuda wa kanisa. Kitabu hiki kifupi, rahisi kusoma, kinaonyesha jinsi theolojia nzuri inavyoleta mabadiliko, uzima, na furaha.
“Kimeandikwa vizuri, chenye kuchochea fikra, na chenye mafundisho ya kiutendaji—Jamieson ameandika hazina ya thamani.”
MARK DEVER, Mchungaji Mkuu, Capitol Hill Baptist Church, Washington, DC
“Maandiko ni kwa ajili ya mafundisho yenye afya, mafundisho yenye afya ni kwa ajili ya maisha halisi, na maisha halisi ni kwa ajili ya ukuaji halisi wa kanisa. Hayo ndiyo Jamieson anasema, na kila mara anapigilia msumari kichwani kwa ustadi mkubwa.”
J. I. PACKER, Profesa wa Theolojia, Regent College
“Jamieson anatufundisha jinsi mafundisho yenye afya yanavyounda na pia kuimarisha huduma zote katika kanisa la mahali, kuanzia uinjilisti wa ufanisi hadi vikundi vidogo vyenye ushirika wa kweli.”
J. D. GREEAR, Mchungaji Kiongozi, The Summit Church, Durham, North Carolina
BOBBY JAMIESON (PhD, Chuo Kikuu cha Cambridge) ni mchungaji msaidizi wa Capitol Hill Baptist Church huko Washington, DC. Awali, aliwahi kuwa mhariri msaidizi wa 9Marks. Jamieson na mke wake wana watoto watatu.
Mafundisho Sahihi: Jinsi Kanisa Linavyokua Katika Upendo na Utakatifu wa Mungu
BOBBY JAMIESON
We do not provide refunds or accept returns for purchased books. However, we are committed to addressing any issues related to manufacturing defects in the books you receive.
