Aibu ya Ushindi wa Msalaba
- Dalvin Mwamakula
- Nov 14
- 2 min read

[Kristo] hakujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama vile kuhani mkuu aingiavyo mahali patakatifu kila mwaka akiwa na damu isiyo yake; ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu” Lakini kama ilivyo sasa, yeye ameonakana mara moja tu katika mwisho wa nyakati ili aondoe dhambi kwa dhabihu yake mwenyewe. (Waebrania 9:25-26)
Haipaswi kuchukuliwa kirahisi kwamba kuwe na makaribisho kwa wenye dhambi mbinguni.
Mungu ni mtakatifu na msafi na mwenye haki kabisa na mkamilifu. Bado hadithi nzima ya Biblia ni jinsi Mungu mkuu na mtakatifu kama huyu anavyoweza na kuwakaribisha watu wachafu, wasio watakatifu kama wewe na mimi katika kibali chake. Hili linawezekanaje?
Waebrania 9:25 inasema kwamba dhabihu ya Kristo kwa ajili ya dhambi haikuwa kama dhabihu za wakuu wa makuhani wa Kiyahudi. Walifika patakatifu kila mwaka wakiwa na dhabihu za wanyama ili kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu. Lakini mistari hiyo inasema kwamba Kristo hakuingia mbinguni ili “kujitoa tena na tena . . . maana ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Waebrania 9:26).
Ikiwa Kristo alifuata kielelezo cha makuhani, basi ingemlazimu kufa kila mwaka. Na kwa kuwa dhambi zitakazofunikwa ni pamoja na dhambi za Adamu na Hawa, ingembidi aanze kufa kwake kila mwaka tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu. Lakini mwandishi anachukulia hii kama jambo lisilofikirika.
Kwanini hili halifikiriki? Kwa sababu ingefanya kifo cha Mwana wa Mungu kionekane dhaifu na kisichofaa. Ikiwa itabidi irudiwe mwaka baada ya mwaka kwa karne nyingi, ushindi ungekuwa wapi? Tungeona wapi thamani isiyo na kikomo wa dhabihu ya Mwana wa Mungu? Ingetoweka katika aibu ya mateso na kifo cha kila mwaka.
Kulikuwa na aibu msalabani, lakini ilikuwa ni aibu ya ushindi. “[Yesu aliidharau] aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu” (Waebrania 12:2).
Hii ndiyo injili ya utukufu wa Kristo, sura ya Mungu (2 Wakorintho 4:4).
“Ninaomba kwamba, hata ukiwa umefunikwa na uchafu wa dhambi kiasi gani, utaona mwanga wa utukufu huu na kuamini.”




Comments