Aina Bora ya Utumwa
- Dalvin Mwamakula
- Jan 27
- 2 min read

Yeye aliyeitwa katika Bwana kama mtumwa ni mtu huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye aliyekuwa huru alipoitwa ni mtumwa wa Kristo. (1 Wakorintho 7:22, tafsiri yangu)
Ningemtarajia Paulo abadilishe mahali pa “Bwana,” ambapo inamaanisha Bwana, na “Kristo,” ambayo inamaanisha Masihi.
Anahusianisha ukombozi wetu na Yesu kuwa Bwana wetu (“mtu huru wa Bwana”). Na anahusianisha utumwa wetu mpya na Yesu kuwa Masihi wetu (“mtumwa wa Kristo”). Inaonekana ajabu kwa sababu Masihi alikuja kuwakomboa watu wake kutoka kwenye utumwa wao; na mabwana huchukua udhibiti wa maisha ya watumwa wao.
Kwanini anasema hivi? Kwanini kuunganisha utumwa (badala ya ukombozi) na Masihi, na ukombozi (badala ya utumwa) na Bwana?
Pendekezo: Kubadili kuna athari mbili kwa uhuru wetu mpya na athari mbili kwa utumwa wetu mpya.
Kwa upande mmoja, kwa kutuita “watu huru wa Bwana ,” analinda na kuweka mipaka uhuru wetu mpya:
1. Ubwana wake uko juu ya mabwana wengine wote; kwa hivyo ukombozi wetu haupingwi- ni salama kabisa.
2. Lakini, tukiwa huru kutoka kwa mabwana wengine wote, hatuko huru kutoka kwake. Uhuru wetu una mipaka kwa rehema. Yesu ni Bwana wetu.
Ubwana wa Yesu uko juu ya mabwana wote; ukombozi wetu upo salama. Uhuru wetu una mipaka kwa rehema zake. Yesu ni Bwana wetu.
Kwa upande mwingine, anapotuita “watumwa wa Kristo,” analegeza na kufanya tufurahie utumwa wetu.
1. Masihi anawadai walio wake ili kuwatoa kutoka kwenye vifungo vya utumwa na kuwaingiza katika maeneo ya wazi ya amani. “Maongezi ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho” (Isaya 9:7).
2. Na huwafanya kuwa wake ili kuwapa furaha tamu zaidi. “Kwa asali ya mwamba ningekushibisha” (Zaburi 81:16). Na Mwamba huo ni Kristo, Masihi.
Kwa hivyo, Mkristo, furahi katika hili: "Yeye aliyeitwa katika Bwana kama mtumwa ni mtu huru wa Bwana " - Bwana. "Vivyo hivyo yeye ambaye alikuwa huru alipoitwa ni mtumwa wa Kristo" - Masihi anayelegeza, aletaye furaha.




Comments