top of page

Aina Mbili za Upinzani kwa Yesu

  • Writer: Joshua Phabian
    Joshua Phabian
  • Dec 5
  • 2 min read
ree

  

Mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye. (Mathayo 2:3)


Yesu anawasumbua watu ambao hawataki kumwabudu, na anachochea upinzani dhidi ya wale wanaomwabudu. Hili pengine sio jambo kuu katika akili ya Mathayo, lakini ni maana isiyoepukika kadiri hadithi inavyoendelea.


Katika hadithi hii, kuna aina mbili ya watu ambao hawataki kumwabudu Yesu.

Aina ya kwanza ni watu wasiofanya lolote kuhusu Yesu. Yeye si kitu katika maisha yao. Kundi hili linawakilishwa mwanzoni mwa maisha ya Yesu na wakuu wa makuhani na waandishi. Mathayo 2:4 inasema, “Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, [Herode] akawauliza ni wapi Kristo angezaliwa.” Kwahiyo wakamwambia, basi: waka kurudi kwenye biashara kama kawaida. Ukimya mtupu na kutojishugulisha kwa viongozi ni balaa kwa kuzingatia ukubwa wa yale yaliyokuwa yanaendelea.


Aina ya pili ya watu ambao hawataki kumwabudu Yesu ni wale ambao wanatishwa sana naye.

Na angalia, Mathayo 2:3 inasema, “Mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye.” Kwa maneno mengine, uvumi ulikuwa ukizunguka kwamba mtu fulani alifikiri Masihi alizaliwa. Kutojishugulisha kwa wakuu wa makuhani kunashangaza: kwa nini usiende na mamajusi? Hawapendi. Hawana shauku ya kumtafuta Mwana wa Mungu na kumwabudu. 


Aina ya pili ya watu ambao hawataki kumwabudu Yesu ni wale ambao wanatishwa sana naye. Huyo ndiye Herode katika hadithi hii. Anaogopa kweli kweli. Kiasi kwamba anapanga njama na kusema uongo na kisha kufanya mauaji ya watoto wengi ili tu kumwondoa Yesu.

Kwa hiyo leo, aina hizi mbili za upinzani zitakuja dhidi ya Kristo na waabudu wake: kutojali na uadui. Hakika ninatumai kuwa hauko katika mojawapo ya vikundi hivyo.

Na kama wewe ni Mkristo, acha Krismasi hii iwe wakati wa kutafakari maana yake gharama yakekuabudu na kumfuata Masihi huyu.





Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page