Aina ya Baridi Inayouaa
- Dalvin Mwamakula
- Jan 27
- 2 min read

Huipeleka amri yake duniani; neno lake hukimbia upesi. (Zaburi 147:15)
Usiku wa leo kutakuwa na joto la digrii arobaini katika friji yetu ya jikoni kuliko ilivyo nje hapa Minneapolis. Halijoto ya juu kesho itakuwa digrii tano chini ya sifuri (Fahrenheit). Tunapokea haya kutoka katika mkono wa Bwana.
Huipeleka amri yake duniani; neno lake hukimbia upesi. Anatoa theluji kama sufu; anatawanya baridi kama majivu. Hurusha chini fuwele zake za barafu kama makombo; ni nani awezaye kusimama mbele ya baridi yake? Hulituma neno lake, na kuviyeyusha; huvumisha upepo wake na maji kutiririka. (Zaburi 147:15-18)
Hii ni aina ya baridi usioweza kucheza nayo. Inaua. Nilipokuja Minnesota kutoka South Carolina, nilivaa kwa ajili ya baridi hii. Lakini sikutayarisha usaidizi wa kuokoa maisha katika gari langu likiharibika.
Jumapili moja usiku nikiwa njiani kurudi kutoka kanisani, katika baridi ya namna hii, gari langu liliharibika. Hii ilikuwa kabla ya simu za mikononi. Nilikuwa na mke na watoto wawili wadogo kwenye gari.
Hakukuwa na mtu kwenye barabara hii. Niligundua ghafla, hii ni hatari.
Muda si muda ilikuwa hatari sana. Hakuna aliyekuja.
Mungu anasema, “Iwe joto, au baridi, juu, au chini, ukali, au ubutu, sauti kubwa, au tulivu, angavu, au giza . . . usicheze na mimi. Mimi ni Mungu. Niliviumba vitu hivi vyote."
Niliona nyumba kwa mbali kupitia uzio. Mimi ndiye baba. Hii ni kazi yangu. Nilipanda uzio na kukimbilia nyumbani na kugonga mlango. Walikuwa nyumbani. Nilieleza kwamba nilikuwa na mke na watoto wawili wadogo ndani ya gari, na nikauliza ikiwa wataturuhusu tuingie. Walifanya hivyo.
Hii ni aina ya baridi ambayo hupaswi kucheza nayo.
Ni njia nyingine ambayo Mungu anasema, “Kama moto au baridi, juu au chini, mkali au butu, sauti kubwa au utulivu, angavu au giza . . . usicheze na mimi. Mimi ni Mungu. Nilifanya vitu hivi vyote.
Vitu hivyo huzungumza kuhusu mimi, kama vile upepo wa kiangazi wenye joto, na mvua nyororo, na usiku mwepesi wa mwezi, na kuvuma kando ya ziwa, na maua ya kondeni na ndege wa angani.”
Kuna neno kwa ajili yetu katika baridi hii. Bwana atupe ngozi ya kuhisi na masikio ya kusikia.




Comments