top of page

Andaa Njia

  • Writer: Joshua Phabian
    Joshua Phabian
  • Dec 2
  • 2 min read
ree

Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao. Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama ya Elia. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake.”. (Luka 1:16-17)


Kile Yohana Mbatizaji alichofanya kwa ajili ya Israeli, Majilio yanaweza kutufanyia. Usiruhusu Krismasi ikukute hujajiandaa. Namaanisha bila kujiandaa kiroho. Furaha yake na athari itakuwa kubwa zaidi ikiwa uko tayari!

Krismasi haitakuwa na athari iliyokusudiwa hadi tuhisi uhitaji mkubwa wa Mwokozi.

Ili uwe umejiandaa . . . 


Kwanza, tafakari juu ya ukweli kwamba tunahitaji Mwokozi. Krismasi ni hati ya mashtaka kabla ya kuwa furaha. “Leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana” (Luka 2:11). Ikiwa hauitaji Mwokozi, hauitaji Krismasi. Krismasi haitakuwa na athari iliyokusudiwa hadi tuhisi uhitaji mkubwa wa Mwokozi. Acha tafakari hizi fupi za Majilio zisaidie kuamsha ndani yako hisia chungu tamu ya hitaji la Mwokozi.


Pili, jihusishe na kujichunguza kibinafsi kwa uharisia. Majilio ni kwa Krismasi kama Kwaresima kwa Pasaka. “Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu; Nijaribu na ujue mawazo yangu! Na uone kama iko njia mbaya ndani yangu, na uniongoze katika njia ya milele! (Zaburi 139:23–24). Hebu kila moyo umtayarishie chumba . . . kwa kusafisha nyumba.


Tatu, jenga matarajio, tazamio linalozingatia Mungu  na hamasa ndani ya nyumba yako - hasa kwa watoto. Ikiwa unahamasa kuhusu Kristo, watakuwa nayo pia. Ikiwa unaweza tu kuifanya Krismasi ya kusisimua kwa vitu vya kimwili, watoto watapataje kiu ya Mungu? Pindua juhudi za mawazo yako ili kufanya maajabu ya kuwasili kwa Mfalme kuonekana kwa watoto.


Nne, kuwa sana katika Maandiko, na kukariri mafungu makuu! Je! neno langu sio kama moto, asema Bwana? (Yeremia 23:29) Kusanyeni moto huo msimu huu wa Majilio. Ni joto. Inameta kwa rangi za neema. Ni uponyaji kwa maelfu ya maumivu. Ni nuru kwa usiku mwingi wa giza.


Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page