top of page

Bora Kuliko Kilimanjaro

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Mar 31
  • 1 min read

Updated: Apr 3

Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. (Warumi 8:28)


Ukiishi ndani ya ahadi hii kubwa, maisha yako ni imara na thabiti kuliko Mlima Kilimanjaro.

 

Hakuna kiwezacho kukuteteresha ukiwa ndani ya uzio wa kuta za Warumi 8:28. Nje ya Warumi 8:28, yote ni mchanganyiko na wasiwasi na hofu na kutokuwa na uhakika. Nje ya ahadi hii ya Mungu inayojumuisha yote ya neema ya baadaye, kuna nyumba za madawa ya kulevya na picha za ngono na mitazamo mingi isiyo na maana. Kuna kuta za mbao na paa za bati za mikakati dhaifu ya uwekezaji, bima za muda mfupi, na mipango ya kustaafu isiyo na maana. Kuna ngome za maboksi zenye kufuli, mifumo ya alamu ya kengele, na makombora ya kuzuia makombora ya masafa marefu. Huko nje kuna mibadala zaidi ya elfu moja ya Warumi 8:28.

 

Unapoingia kupitia mlango wa upendo katika muundo mkubwa na usioweza kutikisika wa Warumi 8:28, kila kitu kinabadilika. Maishani mwako huja utulivu, kina, na uhuru. Ambapo huwezi kuyumbishwa tena. Ujasiri kwamba Mungu mwenye enzi anatawala kwa manufaa yako; maumivu yote na furaha yote utakayopitia ni kimbilio lisilolinganishwa, usalama, tumaini, na nguvu maishani mwako.

 

Watu wa Mungu wanapoishi kwa neema ya baadaye ya Warumi 8:28 — kutoka surua hadi chumba cha kuhifadhia maiti — wanakuwa watu huru zaidi, wenye nguvu zaidi, na wakarimu zaidi duniani.

 

Nuru yao inang’aa na watu wanamtukuza Baba yao aliye mbinguni (Mathayo 5:16).

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page