Dawa kwa ajili ya Mmishonari
- Dalvin Mwamakula
- Oct 15
- 1 min read

Yote yanawezekana kwa Mungu. (Marko 10:27)
Neema kuu ya Mungu ni chemchemi ya maisha kwa Mkristo anayependa furaha kuu [Mdedonisti wa Kikristo]. Kile ambacho mhedonisti anapenda zaidi ni uzoefu wa neema kuu ya Mungu kumjaza, na kutiririka kwa ajili ya wema wa wengine.
Wamishonari wa wenye Uhedonisti wa Kikristo wanapenda uzoefu wa kusema “si mimi, bali neema ya Mungu iliyo pamoja nami” (1 Wakorintho 15:10). Wanajivunia ukweli kwamba matunda ya kazi yao ya kimishonari ni ya Mungu kabisa (1 Wakorintho 3:7; Warumi 11:36).
Wanahisi furaha tu wakati Bwana anaposema, “Bila mimi hamuwezi kufanya chochote” (Yohana 15:5). Wanashangilia kama wanakondoo juu ya ukweli kwamba Mungu ameondoa uzito usiowezekana wa uumbaji mpya kutoka mabegani mwao na kuuweka juu yake mwenyewe. Bila kinyongo, wanasema, “Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu” (2 Wakorintho 3:5).
Wanaporudi nyumbani kwa ajili ya likizo, hakuna kitu kinachowapa furaha zaidi kuliko kusema kwa makanisa, “Sitathubutu kusema chochote isipokuwa kile ambacho Kristo amefanya kupitia mimi ili kuwaleta watu wa mataifa katika utiifu” (Warumi 15:18).
“Mambo yote yanawezekana kwa Mungu!” — mbele maneno hayo yanatoa tumaini, na nyuma yanatoa unyenyekevu. Hayo ni tiba ya kukata tamaa na tiba ya kiburi — dawa kamili ya wamishonari.




Comments