top of page

Dhambi, Shetani, Ugonjwa, au Hujuma

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 15
  • 2 min read
ree

Mara tatu nilimsihi Bwana kuhusu hili, ili liondoke kwangu. Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa nguvu zangu zinakamilishwa katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajivunia udhaifu wangu kwa furaha zaidi, ili nguvu za Kristo zipate kukaa juu yangu. (2 Wakorintho 12:8–9)

 

Je, uchungu unaomjia Mkristo kwa sababu ya mateso ya imani ni sawa na uchungu unaotokana na saratani? Je, ahadi zinazotolewa kwa mmoja zinatumika kwa mwingine? Jibu langu ni ndio. Maisha yote, ikiwa yanaishwi kwa bidii kwa imani katika kutafuta utukufu wa Mungu na wokovu wa wengine, yatakutana na aina fulani ya kikwazo na mateso. Mateso yanayomjia Mkristo mtiifu ni sehemu ya gharama ya kuishi mahali ulipo kwa utii kwa wito wa Mungu.

 

Kwa kuchagua kumfuata Kristo kwa njia anayoelekeza, tunachagua yote ambayo njia hii inajumuisha chini ya riziki Zake kuu.


Hivyo, mateso yote yanayokuja katika njia ya utii ni mateso pamoja na Kristo na kwa ajili ya Kristo iwe ni saratani ukiwa nyumbani au kuteswa ukiwa mbali.

 

Na ni “ ya kuchaguliwa” — yaani, tunachukua kwa hiari njia ya utii ambapo mateso yanatupata, na hatulalamiki dhidi ya Mungu. Tunaweza kuomba — kama Paulo alivyofanya — kwamba mateso yaondolewe (2 Wakorintho 12:8); lakini ikiwa Mungu anataka, tunayakubali kama sehemu ya gharama ya kuwa wanafunzi katika njia ya utii kuelekea mbinguni.

 

Majaribu yote ya mateso katika njia ya utii wa Kikristo, iwe ni kutokana na mateso, ugonjwa au ajali, yana jambo hili moja la kufanana: Yote yanatishia imani yetu katika wema wa Mungu, na kutujaribu kuacha njia ya utii.

 

Kwa hiyo, kila ushindi wa imani, na uvumilivu wote katika utii, ni ushuhuda wa wema wa Mungu na thamani ya Kristo — iwe adui ni ugonjwa, Shetani, dhambi, au hujuma. Kwa hiyo, mateso yote, ya aina yoyote, tunayo vumilia katika njia ya wito wetu wa Kikristo ni mateso “pamoja na Kristo” na “kwa ajili ya Kristo.”

 

Pamoja naye kwa maana kwamba mateso yanatufikia tunapo tembea naye kwa imani, na kwa maana kwamba yanavumiliwa kwa nguvu anazotupatia kupitia huduma yake ya ukuhani mkuu wa huruma kwetu (Waebrania 4:15).

 

Na kwa ajili yake kwa maana kwamba mateso yanajaribu na kuthibitisha uaminifu wetu kwa wema na nguvu zake, na kwa maana kwamba yanaonyesha thamani yake kama fidia na tuzo timilifu kabisa.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page