top of page

Fungate Lisiloisha Kamwe

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • May 29
  • 1 min read

Kama vile bwana harusi anavyomfurahia bibi-arusi, ndivyo Mungu wako atakavyofurahi juu yako. (Isaya 62:5)


Mungu anapowatendea mema watu wake, sio kama hakimu mwenye kusitasita kumtendea kwa fadhili mhalifu anayemwona kuwa mwenye kudharauliwa. Ni kama bwana harusi akionyesha upendo kwa bibi arusi wake. 

 

Wakati mwingine tunatania na kusema juu ya ndoa, “fungate limekwisha.” Lakini hiyo ni kwa sababu sisi tuna mwisho. Hatuwezi kudumisha kiwango kikubwa cha upendo wa fungate. Lakini Mungu anasema kwamba furaha yake juu ya watu wake ni kama bwana arusi juu ya bibi arusi. Na haimaanishi ianze hivyo kisha inafifia.

 

Anazungumza juu ya kina cha fungate na raha za fungate na nguvu ya fungate na msisimko na shauku na starehe. Anajaribu kuingiza ndani ya mioyo yetu kile anachomaanisha anaposema anafurahi juu yetu kwa moyo wake wote. Yeremia 32:41 “Nitafurahi katika kuwatendae mema, nami nitawapanda katika nchi hii kwa uaminifu, kwa moyo wangu wote na kwa roho yangu yote.” Sefania 3:17, “Bwana, Mungu wako, yu katikati yako, shujaa awezaye kuokoa; atakushangilia kwa furaha; atakutuliza kwa upendo wake; atakushangilia kwa kuimba kwa sauti kuu.”

 

Kwa Mungu, fungate haina mwisho. Yeye hana mwisho katika uwezo na hekima na ubunifu ili kusiwe na kuchoka kwa enzi trilioni za milenia zijazo.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page