Furaha Kuu ya Upendo
- Dalvin Mwamakula
- Oct 7
- 2 min read

Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote, bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea kanisa, kwa maana sisi ni viungo vya mwili wake. (Waefeso 5:29-30)
Usikose msemo huo wa mwisho: “kwa sababu sisi tu viungo vya mwili wake.” Na usisahau yale ambayo Paulo alisema mistari miwili mapema, yaani, kwamba Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu “ili alitoe kanisa kwake katika fahari.” Kwa njia mbili tofauti, Paulo anaeleza wazi kwamba Kristo alitafuta furaha yake kwa kutafuta utakatifu, uzuri, na furaha ya watu wake.
Muungano kati ya Kristo na bibi-harusi wake ni wa karibu sana (“mwili mmoja”) yaani kwamba wema wowote anaotendewa ni jambo jema kwake mwenyewe. Hii inamaanisha kwamba tamko la wazi la maandiko haya ni kwamba Bwana anachochewa kumlisha, kumtunza, kumtakasa, na kumsafisha bibi harusi wake kwa sababu katika hili anapata furaha yake.
Kwa fafanuzi zingine, hii haiwezi kuwa upendo. Wanasema, upendo lazima usiwe na ubinafsi—hasa upendo kama wa Kristo, hasa upendo wa Kalvari. Sijawahi kuona mtazamo wa upendo kama huu ukilinganishwa na kifungu hiki cha Maandiko.
Lakini kile ambacho Kristo anafanya kwa bibi-harusi wake, andiko hili linaita upendo waziwazi: “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda kanisa . . . ” (Waefeso 5:25). Kwa nini tusiruhusu maandiko yatufafanulie upendo, badala ya kuleta tafsiri yetu kutoka kwa maadili au falsafa? Kulingana na kifungu hiki, upendo ni kutafuta furaha ya Kristo katika furaha takatifu ya mpendwa.
Hakuna njia ya kuondoa maslahi binafsi kutoka katika upendo, kwa sababu maslahi binafsi si sawa na ubinafsi.
Ubinafsi unatafuta furaha ya kibinafsi kwa gharama ya wengine. Upendo kama wa Kristo unatafuta furaha yake katika furaha ya wengine - si kwa gharama zao.
Utakubali hata kuteseka na kufa kwa ajili ya mpendwa ili furaha yake iweze kutimilika katika maisha na usafi wa mpendwa.
Hivi ndivyo Kristo alivyotupenda, na hivi ndivyo anavyotuita tupendane.




Comments