top of page

Furaha Ya Mungu Kukutendea Mema

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jun 30
  • 2 min read
ree

“Msiogope, enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa ninyi ufalme.” (Luka 12:32)

 

Yesu hataketi oembeni na kutuacha tusiamini bila kupigana. Anachukua silaha ya neno na kunena kwa nguvu kwa wote wanaopata shida ya kuamini.

 

Lengo lake ni kushinda hofu kwamba Mungu si Mungu ambaye kweli anataka kututendea mema — kwamba si mkarimu, msaidizi, mwema, na mpole kwa kweli, bali kwa asili amekasirika nasi — hana nia njema na ametujia kwa hasira.

 

Wakati mwengine, hata ikiwa tunaamini akilini mwetu kwamba Mungu ni mwema kwetu, tunaweza kuhisi moyoni mwetu kwamba wema wake kwa namna fulani umelazimishwa au kushinikizwa, kama hakimu ambaye ameongozwa na wakili mwerevu kwenye kona kwa ufundi fulani, kwenye mahakama, kwa hivyo inambidi afute mashtaka dhidi ya mfungwa ambaye angependelea kumpeleka jela.

 

Lakini Yesu anajitahidi sana kutusaidia tusimhisi Mungu kwa namna hiyo. Katika Luka 12:32, anajitahidi kutufunulia thamani isiyoelezeka na ukuu wa nafsi ya Mungu kwa kuonyesha furaha isiyo na mipaka anayopata katika kutupa Ufalme.

 

“Msiogope, enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa ninyi ufalme.”

 

Kila neno dogo katika sentensi hii ya kushangaza limekusudiwa kusaidia kuondoa hofu ambayo Yesu anajua tunapambana nayo; yaani, kwamba Mungu huwapa watu wake baraka kwa mashaka au kwa kulazimika; kwamba anatenda mema kwa shinikizo, si kwa hulka yake; kwamba kwa undani wake ni mwenye hasira na hupenda kuionyesha.

 

Luka 12:32 ni sentensi inayozungumzia asili ya Mungu. Inazungumzia aina ya moyo alio nao Mungu. Ni mstari unaoonyesha nini humletea Mungu furaha — si tu kile anachofanya au anacholazimika kufanya, bali kile anachopenda kufanya, anachofurahia kufanya, na anachokifurahia kwa moyo wake wote. Kila neno lina uzito wake: “Msiogope, kundi dogo, kwa maana Baba yenu amependezwa kuwapa Ufalme.”

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page