top of page

Furaha ya Yesu katika Ndoa

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 7
  • 2 min read
ree

Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake, ili makusudi alitakase, akiisha kulisafisha kwa maji katika neno, apate kulileta kanisa mbele yake katika fahari. (Waefeso 5:25-27)

 

Sababu ya kuwa na taabu nyingi katika ndoa si kwamba waume na wake wanatafuta raha zao wenyewe, bali ni kwamba hawatafuti raha hiyo katika furaha ya wenzi wao. Agizo la kibiblia kwa waume na wake ni kutafuta furaha yako mwenyewe katika furaha ya mwenzi wako.

 

Hakuna fungu linalochochea mtazamo wa furaha ya Kikristo [Christian Hedonism] zaidi katika Biblia kuliko lile la ndoa katika Waefeso 5:25–30. Waume wanaambiwa wawapende wake zao kama jinsi Kristo alivyolipenda kanisa. 

 

Ni jinsi gani alilipenda kanisa? Mstari wa 25 unasema “alijitoa kwa ajili yake.” Lakini kwanini? Mstari wa 26 unasema, “ili amtakase” na kumsafisha. Lakini kwa nini alitaka kufanya hivyo? Mstari wa 27 unajibu,“ili alitoe kanisa kwake katika fahari!” 

 

Ah! Hiyo hapo! “Kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake [aliustahimili msalaba]” (Waebrania 12:2). Furaha gani? Furaha ya ndoa kwa bibi harusi wake, kanisa. Furaha ya kuwasilisha kanisa kwake katika fahari iliyonunuliwa kwa damu.

 

Unapompenda mtu ambaye Mungu amekufanya kuwa mwili mmoja, unajipenda mwenyewe. Yaani, furaha yako kuu inapatikana katika kutafuta furaha kuu ya mwenzi wako.

Yesu hataki kuwa na mke mchafu na asiye mtakatifu. Kwa hiyo, alikuwa tayari kufa ili kumtakasa na kumsafisha mchumba wake ili aweze kujiletea mke “katika utukufu.” Alipata haja ya moyo wake kwa kujitoa kwenye mateso kwa ajili ya wema wa bibi harusi wake.

 

Kisha Paulo anatumia hili kwa waume katika mistari 28–30: “Vivyo hivyo waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Anayempenda mke wake anajipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea kanisa; kwa maana sisi tu viungo vya mwili wake.” 

 

Yesu alikuwa amewaambia waume na wake - na wengine wote - "Mpende jirani yako kama nafsi yako" (Mathayo 22:39). Ndoa ni mahali pa kipekee pa vitendo. Sio tu "kama" unavyojipenda mwenyewe. Lakini unajipenda mwenyewe. Unapompenda mtu ambaye Mungu amekufanya kuwa mwili mmoja, unajipenda mwenyewe. Yaani furaha yako kuu inapatikana katika kutafuta furaha kuu ya mwenzi wako.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page