top of page

Hatari ya Kupotoka

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 15
  • 1 min read
ree

Kwa hiyo, tunapaswa kutilia maanani zaidi yale tuliyosikia, tusije tukayapoteza. (Waebrania 2:1)

 

Sote tunawajua watu ambao hili limewatokea. Hakuna uharaka. Hakuna uangalizi. Hakuna kusikiliza kwa umakini, kutafakari, au kumtazama Yesu. Na matokeo hayakuwa kusimama tu, bali ni kupeperushwa mbali.

 

Hapo ndipo hoja ilipo: hakuna kusimama tu. Maisha ya dunia hii si ziwa. Ni mto. Na unatiririka kuelekea uharibifu. Usipomsikiliza Yesu kwa bidii na kumfikiria kila siku na kumtazama kila saa, hutasimama tu; utarudi nyuma. Utaelea mbali na Kristo.

 

Maisha ya dunia hii si ziwa, ni mto unaotiririka kuelekea uharibifu. Usipomsikiliza Yesu kwa bidii na kumtazama kila saa, hutosimama ulipo, utarudi nyuma na kuelea mbali na Kristo.

Kupotoka ni jambo hatari katika maisha ya Kikristo. Na tiba yake, kulingana na Waebrania 2:1, ni: Sikiliza kwa makini kile ulichosikia. Yaani, fikiria kile Mungu anachosema kupitia Mwana wake Yesu. Kazia macho kile Mungu anachosema na kufanya kupitia Mwana wa Mungu, Yesu Kristo. 

 

Hii si mbinu ngumu ya kuogelea kujifunza. Kitu pekee kinachotuzuia kuogelea kinyume na utamaduni wa dhambi si ugumu wa mbinu, bali ni tamaa yetu ya dhambi ya kwenda na mkondo. 

 

Tusilalamike kwamba Mungu ametupa kazi ngumu. Sikiliza, fikiria, tazama kwa makini — hii huwezi kuita ni maelezo magumu ya kazi. Kiuhalisia, haya siyo maelezo ya kazi. Ni mwaliko wa dhati kuridhika katika Yesu ili tusivutwe na tamaa za udanganyifu.

 

Ikiwa unapotoka leo, moja ya ishara za matumaini kwamba umeokoka ni kwamba unahisi kuchomwa kwa hili, na unahisi hamu inayoongezeka ya kumgeukia Yesu na kumfikiria na kumsikiliza katika siku, miezi, na miaka ijayo.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page