top of page

Hatuwezi Kufanya Chochote

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 7
  • 2 min read
ree

“Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” (Yohana 15:5)


Tuseme umepooza kabisa na huwezi kujifanyia chochote isipokuwa kuzungumza. Na fikiria rafiki mwenye nguvu na wa kuaminika anaahidi kuishi na wewe na anafanya chochote unachohitaji kifanyike. Unawezaje kumtukuza rafiki huyu ikiwa mgeni atakuja kukuona? 


Je, ungemtukuza kwa ukarimu wake na nguvu zake kwa kujaribu kutoka kitandani na kumbeba? Hapana!  Ungesema, “Rafiki, tafadhali njoo uniinue, na unaweza kuweka mto nyuma yangu ili niweze kumwangalia mgeni wangu? Na tafadhali unaweza kunivalisha miwani yangu?” 


Na hivyo mgeni wako ange jifunza kutoka kwa maombi yako kwamba wewe huna msaada na kwamba rafiki yako ni mwenye nguvu na mkarimu. Unamtukuza rafiki yako kwa kumhitaji, kumwomba msaada, na kumtegemea.


Katika Yohana 15:5, Yesu anasema, “Pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” Kwa hiyo kweli tumepooza. Bila Kristo, hatuwezi kufanya lolote linalomtukuza Kristo. Kama vile Paulo asemavyo katika Warumi 7:18 , “Hakikai neno jema ndani yangu, yaani, katika mwili wangu.” 


Tunamwomba Mungu atufanyie sisi kwa njia ya Kristo yale ambayo hatuwezi kujifanyia wenyewe — kuzaa matunda.

Lakini Yohana 15:5 pia anasema kwamba Mungu anakusudia tufanye mema mengi yanayomwinua Kristo, yaani, kuzaa matunda: “Yeye akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo ndiye ambaye huzaa sana.” Kwa hivyo kama rafiki yetu mwenye nguvu na wa kutegemewa—“nimewaita rafiki” ( Yohana 15:15 )—anaahidi kufanya kwa ajili yetu, na kupitia sisi, yale ambayo hatuwezi kujifanyia wenyewe.


Tunamtukuzaje basi? Yesu anatoa jibu katika Yohana 15:7 : “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote, nanyi mtatendewa.” Tunaomba! Tunamwomba Mungu atufanyie sisi kwa njia ya Kristo yale ambayo hatuwezi kujifanyia wenyewe—kuzaa matunda. 

Andiko la Yohana 15:8 linatoa matokeo: “Kwa hili hutukuzwa Baba yangu, kwamba mzae matunda mengi.” 


Kwa hiyo Mungu hutukuzwaje kupitia maombi? Maombi ni kukiri wazi kwamba bila Kristo hatuwezi kufanya lolote. Na sala ni kugeuka kutoka kwetu wenyewe kwenda kwa Mungu kwa ujasiri kwamba atatupa msaada tunaohitaji.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page