Hofu na Tumaini katika Wivu wa Mungu
- Dalvin Mwamakula
- Oct 7
- 2 min read

"Bwana, ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu." ( Kutoka 34:14 )
Mungu ana wivu usio na kikomo kwa heshima ya jina lake, na anajibu kwa ghadhabu kali dhidi ya wale ambao mioyo yao inapaswa kuwa yake lakini wanakimbilia vitu vingine, kama vile mwenzi anayemkimbilia mpenzi mwingine.
Kwa mfano, katika Ezekieli 16:38–40 anawaambia Israeli wasio na imani,
“Nitakuhukumu kama wahukumiwavyo wanawake wazinzi na kumwaga damu, nami nitaleta juu yako damu ya ghadhabu na wivu. Nami nitakutia mikononi mwao, nao watakibomoa chumba chako cha tambarare. . . . Watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vya kupendeza na kukuacha uchi na mtupu. Wataleta umati juu yako, nao watakupiga kwa mawe na kukatoka vipande-vipande kwa panga zao.”
Nakusihi usikilize onyo hili. Wivu wa Mungu kwa upendo wako usio gawanyika na ibada yako daima utakuwa na kauli ya mwisho. Chochote kinachovuta hisia zako mbali na Mungu kwa mvuto wa udanganyifu kitakugeukia na kukuvua nguo na kukukatakata vipande vipande.
Ni jambo la kutisha kutumia maisha uliyopewa na Mungu kufanya uzinzi dhidi ya Mwenyezi.
Wivu wa Mungu ni tishio kwa wanaofanya ukahaba na kuiuza mioyo yao kwa ulimwengu, lakini ni faraja kwa wanaoshika nadhiri za agano na kuwa wageni duniani.
Lakini kwa wale ambao wameunganishwa kweli na Kristo na wanaoshika nadhiri zao za kuacha wengine wote na kushikamana naye tu na kuishi kwa heshima yake — kwenu wivu wa Mungu ni faraja kuu na tumaini kuu.
Kwa kuwa Mungu ana wivu usio na kikomo kwa ajili ya heshima ya jina lake, chochote na yeyote anaye tishia wema wa mke wake mwaminifu atapingwa kwa uwezo wa kimungu. Hiyo ni habari njema kwa mke mwaminifu - watu waaminifu wa Mungu.
Wivu wa Mungu ni tishio kubwa kwa wale wanaofanya ukahaba na kuuza mioyo yao kwa ulimwengu na kufanya chuki kutoka kwa Mungu (Yakobo 4:3-4). Lakini wivu wake ni faraja kuu kwa wale wanaoshika nadhiri zao za agano na kuwa wageni na wakimbizi duniani.




Comments