Imani Humheshimu Yule Inayomwamini
- Dalvin Mwamakula
- May 29
- 1 min read

Lakini Abrahamu hakusitasita kwa kutokuamini ahadi ya Mungu, bali alitiwa nguvu katika imani yake na kumpa Mungu utukufu. (Warumi 4:20)
Lo, jinsi ninavyotamani Mungu atukuzwe katika kutafuta kwetu utakatifu na upendo. Lakini Mungu hatukuzwi isipokuwa kama harakati zetu zinatiwa nguvu na imani katika ahadi zake.
Na Mungu aliyejidhihirisha kikamilifu katika Yesu Kristo, ambaye alisulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuka kwa ajili ya kuhesabiwa haki kwetu (Warumi 4:25), hutukuzwa sana tunapokumbatia ahadi zake kwa uthabiti wa furaha kwa sababu zimenunuliwa kwa damu ya Mwana wake.
Mungu anaheshimiwa tunaponyenyekezwa kwa ajili ya unyonge na kushindwa kwetu, na anapoaminiwa kwa neema ya wakati ujao. Hiyo ndiyo hoja ya Warumi 4:20 ambapo Paulo anafafanua imani ya Ibrahimu, “Kutokuamini hakukumfanya asiwe na shaka juu ya ahadi ya Mungu, bali alitiwa nguvu katika imani akimtukuza Mungu.
Alipata kuongezeka nguvu katika imani yake, na hivyo kumtukuza Mungu. Imani katika ahadi za Mungu humtukuza kuwa mwenye hekima nyingi na mwenye nguvu na mzuri na mwenye kuaminiwa. Kwa hiyo, tusipojifunza jinsi ya kuishi kwa imani katika ahadi za neema ya Mungu ya wakati ujao, tunaweza konyesha mbwembwe za ajabu za kidini, lakini sio kwa utukufu wa Mungu.
Anatukuzwa wakati nguvu ya kuwa mtakatifu inakuja kupitia unyenyekevu wa imani katika neema ya wakati ujao.
Martin Luther alisema,
“[Imani] humheshimu yule inayemwamini kwa heshima ya juu zaidi, kwa kuwa inamwona kuwa mkweli na mwaminifu.”
Mtoaji anayeaminika anapata utukufu.
Nia yangu kubwa ni kwamba tujifunze jinsi ya kuishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Na hiyo inamaana ya kuishi kwa imani katika neema ya wakati ujao, ambayo, kwa upande wake, inamaana ya kupigana na kutokuamini kwa njia zote zinazoinua kichwa chake.




Comments