top of page

Imani Huondoa Hatia, Uchoyo, na Hofu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jun 30
  • 2 min read
ree

Kusudi la maagizo haya ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri safi na imani ya kweli. (1 Timotheo 1:5)

 

Paulo analenga upendo. Na moja ya vyanzo muhimu vya athari hii kubwa ni imani ya kweli. Sababu ya imani kuwa chanzo cha uhakika wa upendo ni kwamba imani katika neema ya Mungu hufukuza nguvu za dhambi kwenye moyo zinazozuia upendo.

 

Tunapojihisi kuwa na hatia, tunaangukia mahala pa kuhisi mgandamizo binafsi  na kujihurumia, bila kuona, sembuse kujali, hitaji la mtu mwingine yeyote. Au tunafanya unafiki ili kufunika hatia yetu, na hivyo kuharibu uaminifu wote katika mahusiano, ambayo hufanya upendo wa kweli usiwezekane. Au tunazungumza juu ya makosa ya watu wengine ili kupunguza hatia yetu wenyewe, s upendo haufanyi hivyo. Kwa hivyo, ikiwa tutapenda, athari haribifu za hatia lazima zishindwe.

 

Ni sawa na hofu. Ikiwa tunahisi kuwa na hofu, tunaelekea kutomkaribia mgeni kanisani ambaye anaweza kuhitaji neno la kukaribishwa na kutia moyo. Au tunaweza kukataa misheni ya mipakani kama wito, kwa sababu inaonekana kuwa hatari sana. Au tunaweza kupoteza pesa kwa kupata bima kubwa kupita kiasi, au kumezwa na aina zote za woga unaotufanya tujishughulishe na kutufanya tusione mahitaji ya wengine. Yote hayo ni kinyume cha upendo.

 

Ni sawa na uchoyo. Ikiwa tuna tamaa, tunaweza kutumia pesa kwa anasa - pesa ambazo zinafaa kwenda kueneza injili. Hatufanyi kitu chochote hatari, isije kuhatarisha mali zetu za thamani na mustakabali wetu wa kifedha. Tunazingatia vitu badala ya watu, au tunaona watu kama rasilimali kwa ajili ya faida zetu za kimwili. Kwa hivyo upendo uharibiwa.

 

Lakini imani katika neema ya wakati ujao huzaa upendo kwa kuondoa hatia na hofu na uchoyo kutoka moyoni.

 

Inasukuma nje hatia kwa sababu inashikilia sana tumaini kwamba kifo cha Kristo kinatosha kupata kuachiliwa na haki sasa na milele (Waebrania 10:14).

 

Inasukuma nje hofu kwa sababu inaegemea ahadi, “Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe. . . . Mimi niitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu” (Isaya 41:10).

 

Na inasukuma nje uchoyo kwa sababu ina uhakika kwamba Kristo ni mali kuu kuliko yote ambayo ulimwengu unaweza kutoa (Mathayo 13:44).

 

Kwa hiyo Paulo anaposema, “Lengo la agizo letu ni upendo utokao kwa . . . imani ya kweli,” anazungumzia uwezo mkubwa wa imani kushinda vizuizi vyote vya upendo. Tunapopigana vita vya imani - vita vya kuamini ahadi za Mungu zinazoua hatia na hofu na uchoyo - tunapigania upendo.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page