top of page

Imani kwa ajili ya Yasiyowezekana

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • May 29
  • 2 min read
ree

Alitiwa nguvu katika imani yake na kumpa Mungu utukufu, akiwa na hakika kabisa kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kutimiza lile aliloahidi. (Warumi 4:20-21)


Paulo anazingatia sababu maalum kwa nini imani hutukuza neema ya Mungu ya wakati ujao. Kwa kifupi, sababu ni kwamba imani hiyo ya kumtukuza Mungu ni tumaini linaloelekezwa wakati ujao katika uaminifu, maadili, nguvu, na hekima ya Mungu ya kutimiza ahadi zake zote. 

 

Paulo anaonyesha imani hii kwa jibu la Ibrahimu kwa ahadi ya Mungu: kwamba atakuwa baba wa mataifa mengi ingawa alikuwa mzee na mke wake alikuwa tasa (Warumi 4:18). “Kwa tumaini aliamini pasipo tumaini,” yaani, alikuwa na imani katika neema ya wakati ujao ya ahadi ya Mungu, licha ya uthibitisho wote wa kibinadamu ulio kinyume chake. 

 

Hakudhoofika katika imani alipoufikiria mwili wake mwenyewe, ambao ulikuwa umekufa (sababu alikuwa na umri wa miaka mia moja hivi), au alipofikiria utasa wa tumbo la uzazi la Sara. Hakuna kutokuamini kulikomfanya apate kusitasita kuhusu ahadi ya Mungu, bali aliimarika katika imani yake akimtukuza Mungu, akiwa na hakika kabisa kwamba Mungu anaweza kufanya yale aliyoahidi. (Warumi 4:19-21)

 

Hii ndiyo imani tunayotakiwa kuwa nayo, kwamba Mungu atatufanyia kile tusichoweza kujifanyia.

Imani ya Ibrahimu ilikuwa imani katika ahadi ya Mungu ya kumfanya kuwa baba wa mataifa mengi. Imani hii ilimtukuza Mungu kwa sababu ilielekeza umakini kwenye rasilimali zote za Mungu muweza-yote, zisizo za kawaida ambazo zingehitajika ili kuitimiza. 

 

Ibrahimu alikuwa mzee sana asingeweza kupata watoto, na Sara alikuwa tasa. Sio hivyo tu: Unawezaje kugeuza mwana au wawili kuwa “mataifa mengi,” ambayo Mungu alisema Ibrahimu angekuwa baba yao? Yote yalionekana kuwa haiwezekani kabisa. 

 

Kwa hiyo, imani ya Ibrahimu ilimtukuza Mungu kwa kuwa na uhakika kamili kwamba angeliweza na angelifanya mambo yasiyowezekana kibinadamu. Hii ndiyo imani tuliyoitwa kuwa nayo. Kwamba Mungu atatufanyia kile ambacho hatungeliweza kujifanyia wenyewe.


Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page