top of page

Ishi kwa Ujasiri katika Nguvu ya Ukuu wa Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 2
  • 1 min read
ree

Ukuu wa uweza wake usiopimika kwetu sisi tunaoamini. . . (Waefeso 1:19)


Uweza wa Mungu unamaanisha kimbilio la milele lisilotikisika katika utukufu wa milele wa Mungu bila kujali kinachotokea duniani. Na ujasiri huo ndio chanzo na nguvu ya utii wa dhati kwa wito wa Mungu. 

 

Je, kuna kitu chochote cha kuweka huru, cha kusisimua zaidi, au kinachotia nguvu zaidi kuliko ukweli kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kimbilio lako - siku nzima, kila siku, katika matukio yote ya kawaida na ya ajabu ya maisha?

 

Kama tungeliamini hili, kama tungeliruhusu kweli hii ya uweza wa Mungu kutushika, ingefanya tofauti kubwa katika maisha yetu binafsi na katika huduma zetu! Ni jinsi gani tungekuwa wanyenyekevu na wenye nguvu kwa makusudi ya kuokoa ya Mungu! 

 

Uweza wa Mungu unamaanisha kimbilio kwa watu wa Mungu. Na unapokuwa na imani ya kweli kwamba kimbilio lako ni uweza wa Mungu Mwenyezi, kuna furaha na uhuru na nguvu inayomwagika katika maisha ya utii wa hali ya juu kwa Yesu Kristo.

 

Uweza wa Mungu unamaanisha heshima, malipo, na kimbilio kwa watu wake wa agano. 

 

Ninakualika ukubali masharti ya agano lake la neema:


Geuka kutoka dhambini na umtumaini Bwana Yesu Kristo; na uweza wa Mungu Mwenyezi utakuwa heshima ya roho yako, malipo ya maadui zako, na kimbilio la maisha yako — milele.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page