Jambo Pekee Liwezalo Kusafisha Dhamiri
- Dalvin Mwamakula
- Nov 14
- 1 min read

Si zaidi sana damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itasafisha dhamira zetu na matendo mafu, tupate kumwabudu Mungu aliye hai? (Waebrania 9:14)
Hapa tuko katika enzi ya kisasa - enzi ya Intaneti, simu mahiri, kusafiri angani, na upandikizaji wa moyo - na shida yetu kimsingi ni sawa na siku zote: Dhamiri zetu hutuhukumu na kutufanya tuhisi kuwa hatukubaliki kwa Mungu. Tumetengwa mbali na Mungu. Na dhamiri zetu zinatushuhudia.
Tunaweza kujikata, au kutupa watoto wetu katika mto mtakatifu, au kutoa dola milioni kwa wenye uhitaji, au kutumikia katika kutoa msaada wa chakula, au aina mia za toba au kujiumiza, na matokeo yatakuwa sawa: Doa linabaki na kifo kinatisha.
Tunajua kwamba dhamiri zetu zimetiwa unajisi - sio kwa vitu vya nje kama kugusa maiti, nepi chafu, au kipande cha nguruwe. Yesu alisema ni kile kitokacho ndani ya mtu ndicho kimtiacho unajisi, sio kile kinachoingia ndani (Marko 7:15–23). Tunanajisika na mitazamo kama kiburi na kujihurumia na uchungu na tamaa na husuda na choyo na kutojali na woga.
Jibu pekee katika wakati huu wa kisasa, kama katika kila wakati mwingine, ni damu ya Kristo. Dhamira yako ikiinuka na kukuhukumu, utageukia wapi?
Waebrania 9:14 inakupa jibu: “Basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itasafisha dhamira zetu na matendo mafu, tupate kumwabudu Mungu aliye hai.
Jibu ni:
Geukia damu ya Kristo. Geukia kitu pekee kinachoweza kutakasa katika ulimwengu, kinachoweza kukupa unafuu katika maisha, na amani katika kifo.




Comments