top of page

Je, Kristo Anastahili?

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 2 min read

Updated: May 1

ree

“Mtu akija kwangu na hamchukii baba yake mwenyewe na mama yake na mke wake na watoto na kaka na dada zake, naam, na hata maisha yake mwenyewe, hawezi kuwa mfuasi wangu. Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake mwenyewe na kuja kwangu hawezi kuwa mfuasi wangu.” (Luka 14:26-27)


Yesu haoni haya na haogopi kutuambia moja kwa moja "mabaya" - gharama na uchungu wa kuwa Mkristo: kuchukia familia (mstari wa 26), kubeba msalaba (mstari wa 27), kukataa mali (mstari wa 33). Hakuna alama ndogo katika agano la neema. Yote ni kubwa, na ya ujasiri. Hakuna neema ya gharama ndogo! Gharama kubwa sana! Njoo uwe mfuasi wangu.


Lakini Shetani huficha ubaya wake na huonyesha ubora wake tu. Yote ambayo ni muhimu sana katika makubaliano na Shetani, yako kwa maandishi madogo kwenye ukurasa wa nyuma.


Katika ukurasa wa mbele herufi kubwa, nzito kuna maneno, “Hakika hutakufa” (Mwanzo 3:4), na “Haya yote nitakupa, ukinsujudu na kuniabudu” (Mathayo 4:9) Lakini katika ukurasa wa nyuma kwa maandishi madogo— sana unaweza kuisoma tu kwa kioo cha kukuza Biblia—inasema, “Na baada ya anasa za kitambo, utateseka pamoja nami milele kuzimu.”


Kwa nini Yesu yuko tayari kutuonyesha “mabaya” yake na vilevile bora zaidi, huku Shetani atatuonyesha yaliyobora tu kuhusu yeye? Matthew Henry anajibu, “Shetani huonyesha kilicho kizuri zaidi, lakini huficha kilicho kibaya zaidi, kwa sababu kilicho kizuri zaidi kwake hakiwezi kufidia ubaya wake; lakini cha Kristo huweza, na zaidi ya hapo.”


Wito wa Yesu sio wito tu wa kuteseka na kujinyima; kwanza ni wito wa kwenda kwenye karamu. Hili ndilo lengo la mfano katika Luka 14:16–24. Yesu pia anaahidi ufufuo wa utukufu ambapo hasara zote za maisha haya zitalipwa (Luka 14:14). Pia anatuambia kwamba atatusaidia kuvumilia katika magumu (Luka 22:32). Pia anatuambia Baba yetu atatupa sisi Roho Mtakatifu (Luka 11:13). Anaahidi kwamba hata kama tutauawa kwa ajili ya ufalme, “hakuna unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea” (Luka 21:18).


Ina maana ya kwamba tunapoketi kuhesabu gharama ya kumfuata Yesu - tunapopima yaliyo "mabaya" na yaliyo "bora" - yeye anastahili. Anastahili sana.


Si hivyo kwa Shetani. Mkate ulioibwa ni mtamu, lakini baadaye kinywa hujaa changarawe (Mithali 20:17).


Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page