top of page

Je, Unamjua Mungu Vizuri kiasi Gani?

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jun 30
  • 1 min read
ree

“Tazama, Mungu ni mkuu, wala hatumjui; hesabu ya miaka yake haitafutiki.” (Ayubu 36:26)


Haiwezekani kumjua Mungu kipita kiasi.

 

Yeye ndiye mtu muhimu kuliko wote wengine. Na hii ni kwa sababu aliviumba vingine vyote, na umuhimu wowote vilivyo navyo ni kwasababu yake, vimetokana naye. Nguvu au akili au ujuzi au uzuri wowote uliopo ndani ya viumbe wengine hutoka kwake. Katika kila kiwango cha ubora, yeye ni mkuu kuliko mtu bora zaidi uliyewahi kumjua au kumsikia.

 

Kwa kuwa hana mwisho, yeye huvutia bila kuchosha. Haiwezekani, basi, kwamba Mungu awe wa kuchosha. Maonyesho yake ya mara kwa mara ya matendo yaliyo ya juu kiakili na ya kuvutia ni kama mlipuko wa volkano.

 

Akiwa chanzo cha kila raha njema, yeye mwenyewe hutosheleza na kuridhisha kabisa. Na ikiwa hatumpati hivyo, basi ama tumekufa, au hatuoni, au tunatembea usingizini.

 

Ni jambo la kushangaza, basi, jinsi jitihada chache sana huwekwa katika ulimwengu huu ili kumjua Mungu.

 

Ni kama vile Rais wa Tanzania angekuja kuishi nawe kwa mwezi mzima, lakini wewe ungemsalimia tu “habari” kwa haraka kila baada ya siku moja au mbili. Au kama vile ungesafiri kwa mwendo wa mwanga kwa saa chache ukizunguka jua na mfumo wa jua, lakini badala ya kutazama nje ya dirisha kuona hayo maajabu, ukachagua kucheza mchezo wa kompyuta. Au kama ungealikwa kutazama waigizaji, waimbaji, wanamichezo, wavumbuzi, na wasomi bora kabisa wakiwasilisha kilele cha vipawa vyao, lakini ukakataa kwenda ili kutazama kipindi cha mwisho cha tamthilia kwenye runinga.

 

Tuombe pamoja kwamba Mungu wetu mkuu asiye na mwisho aelekeze mioyo yetu kwake, na afungue macho yetu ili tumwone kadiri tuwezavyo, na tuwe na shauku ya kumjua zaidi.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page