top of page

Jihadhari na Kumtumikia Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 7
  • 2 min read
ree

“Mungu aliyeufanya ulimwengu na vyote vilivyomo, ambaye ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa na wanadamu, wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu, kwa kuwa yeye ndiye huwapa wanadamu wote uzima na pumzi na kila kitu.” (Matendo 17:24-25)

 

Hatumtukuzi Mungu kwa kumhudumia mahitaji yake, bali kwa kuomba atutimizie yetu — na kutumaini atajibu, na kuishi katika furaha ya ule utunzaji wake wote tunapojitoa maisha yetu kwa upendo kwa watu wengine.

 

Hapa tuko katika kiini cha habari njema ya Ukristo wa 'Hedonism'(Furaha). Msisitizo wa Mungu kwamba tumwombe atusaidie ili apate utukufu. “Uniite siku ya taabu; nitakuokoa, nawe utanitukuza” (Zaburi 50:15). Hii inatufanya tukabiliane na ukweli wa kushangaza kwamba tunapaswa kuwa waangalifu tusifikirie kwamba Mungu anatuhitaji sisi. Ni lazima tuwe waangalifu na kumtumikia Mungu, na tunapaswa kuchukua tahadhari maalum kumruhusu atuhudumie sisi, tusije tukamnyang’anya utukufu wake. “Mungu hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu” (Matendo 17:25). 

 

Hii inaonekana kuwa ya ajabu sana. Wengi wetu tunafikiri kumtumikia Mungu ni jambo chanya kabisa. Hatukufikiria kwamba kumtumikia Mungu kunaweza kuwa tusi kwake. Lakini kutafakari juu ya maana halisi ya maombi hufanya hili kuwa wazi. 

 

Hatumtukuzi Mungu kwa kumhudumia mahitaji yake, bali kwa kuomba atutimizie yetu, kutumaini atajibu, na kuishi kwa furaha tukijitoa kwa upendo kwa wengine.

Katika riwaya ya Robinson Crusoe, shujaa wa riwaya alichukua Zaburi 50:12-15 kama maandiko yake anayopenda kutumaini alipokuwa amekwama kwenye kisiwa: Mungu anasema, “Kama ningekuwa na njaa, nisingelikwambia, kwa maana ulimwengu na vyote vilivyomo ni vyangu. Uniite siku ya taabu; nitakukomboa, na wewe utanitukuza.” 

 

Inamaanisha: kuna njia ya kumtumikia Mungu ambayo inaweza kumdharau kama mhitaji wa huduma yetu. Tunapaswa kuwa waangalifu tusije tukaitangulia neema kuu ya Mungu katika Kristo. Yesu alisema, “Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia kwa wengi” (Marko 10:45). Yeye anakusudia kuwa mtumishi. Anakusudia kupata utukufu kama Mpaji.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page