Jihubirie Mwenyewe
- Dalvin Mwamakula
- Jun 30
- 2 min read

Ee nafsi yangu, kwa nini unanasononeka, na kwa nini unafadhaika ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu; kwa kuwa bado nitamsifu, mwokozi wangu na Mungu wangu. (Zaburi 42:11)
Lazima tujifunze kupambana na hali ya kukata tamaa — roho iliyovunjika moyo. Mapambano haya ni mapambano ya imani katika neema ya baadaye. Tunapambana kwa kujihubiria kweli kuhusu Mungu na ahadi yake ya baadaye.
Hivi ndivyo mtunga-zaburi anafanya katika Zaburi 42. Mtunga-zaburi anaihubiri nafsi yake yenye shida. Anajikanya na kujihoji mwenyewe. Na hoja yake kuu ni neema ya wakati ujao: “Mtumaini Mungu! Mtumaini Mungu atakavyokuwa kwako siku zijazo. Siku ya sifa inakuja. Uwepo wa Bwana utakuwa msaada wote unaohitaji. Naye ameahidi kuwa pamoja nasi milele.”
Martyn Lloyd-Jones anaamini suala hili la kujihubiria ukweli kuhusu neema ya Mungu ya wakati ujao ni muhimu sana katika kushinda huzuni ya kiroho. Katika kitabu chake chenye kusaidia, Spiritual Depression [Sonona ya Kiroho], anaandika, Je, umegundua kwamba sehemu kubwa ya kutokuwa na furaha maishani mwako ni kutokana na ukweli kwamba unajisikiliza badala ya kujisemesha mwenyewe? Chukua mawazo hayo yanayokujia wakati unapoamka asubuhi.
Hujayaanzisha, lakini yanaanza kukusemesha, yanarudisha matatizo ya jana, nk. Mtu anazungumza. . . Wewe mwenyewe unazungumza na wewe. Sasa matibabu ya mtu huyu [katika Zaburi 42] yalikuwa hivi: badala ya kumruhusu mtu huyu kuzungumza naye, anaanza kujisemesha yeye mwenyewe. “Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? anauliza. Nafsi yake ilikuwa ikimfadhaisha, kumponda. Kwa hiyo anasimama na kusema, “Binafsi, sikiliza kwa muda. nitazungumza nawe.” (20–21)
Vita dhidi ya kukata tamaa ni vita ya kuamini ahadi za Mungu. Na imani hiyo katika neema ya Mungu ya wakati ujao inakuja kwa kusikia neno. Na hivyo kujihubiria neno la Mungu ni kiini cha vita.




Comments