top of page

Jinsi Kristo Alivyoushinda Uchungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jun 30
  • 1 min read
ree

Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipotesewa, hakutishia, bali alikabidhi kwa yeye ahukumuye kwa haki. (1 Petro 2:23)


Hakuna aliyetendewa dhambi mbaya zaidi kuliko Yesu. Kila uadui dhidi yake hakuustahili kabisa.

 

Hakuna aliyewahi kuishi ambaye alistahili heshima zaidi kuliko Yesu; na hakuna aliyevunjiwa heshima zaidi yake.

 

Ikiwa mtu yeyote alikuwa na haki ya kukasirika na kuwa na uchungu na kulipiza kisasi, alikuwa ni Yesu. Aliwezaje kujidhibiti wakati walaghai, ambao kuishi kwao kumeshikiliwa naye, walimtemea mate usoni? Andiko la 1 Petro 2:23 linatoa jibu: “Alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteseka, hakutishia, bali aliendelea kujikabidhi kwa yeye ahukumuye kwa haki.”

 

Kristo alishinda uchungu na kisasi kwa imani katika ahadi za Mungu, Hakimu mwema. Je, sisi tunapaswa kufanya nini zaidi, kwa kuwa tuna haki ndogo ya kunung'unika kwa kuteswa kuliko yeye?

Maana ya mstari huu ni kwamba Yesu alikuwa na imani katika neema ya wakati ujao ya hukumu ya haki ya Mungu. Hakuhitaji kujilipiza kisasi kwa ajili ya maovu yote ya kushushiwa hadhi na heshima aliyoteseka, kwa sababu alikabidhi jambo lake kwa Mungu. Aliacha kisasi mikononi mwa Mungu na kuwaombea adui zake: “Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo” (Luka 23:34).

 

Petro anatupa mtazamo huu wa imani ya Yesu ili tujifunze jinsi ya kuishi hivi sisi wenyewe. Alisema, “Umeitwa [kuvumilia mateso makali kwa uvumilivu] . . . kwa maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake” (1 Petro 2:21).

 

Ikiwa Kristo alishinda uchungu na kisasi kwa imani katika yale ambayo Mungu, Hakimu mwema, alikuwa ameahidi kufanya, je, sisi tunapaswa kufanya nini zaidi, kwa kuwa tuna haki ndogo sana ya kunung'unika kwa kuteswa kuliko yeye?



Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page