top of page

Jinsi Shetani Anavyomtumikia Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Nov 12
  • 2 min read
ree

Tazama, tunawaona walio heri waliobaki kuendea kuwa na uthabiti. Mmesikia juu ya uthabiti wa Ayubu, na mmeona kusudi la Bwana, jinsi Bwana alivyo na huruma na rehema. (Yakobo 5:11)

 

Nyuma ya magonjwa yote na ulemavu kuna mapenzi makuu ya Mungu. Sio kwamba Shetani hahusiki - labda daima anahusika kwa njia moja au nyingine na makusudi ya uharibifu (Matendo 10:38). Lakini uwezo wake hautoi uamuzi wa mwisho. Hawezi kutenda bila ruhusa ya Mungu.


Shetani anaweza kuhusika katika shida zetu na makusudi yake ya uharibifu. Lakini uwezo wake hautoi uamuzi wa mwisho. Hawezi kutenda bila ruhusa ya Mungu.

 

Hiyo ndiyo mojawapo ya hoja za ugonjwa wa Ayubu. Andiko hilo linaonyesha wazi kwamba ugonjwa ulipomjia Ayubu, “Shetani . . . akampiga Ayubu kwa vidonda vya kuchukiza” (Ayubu 2:7). Mke wake alimsihi amlaani Mungu. Lakini Ayubu akasema, Je tutapokea mazuri tu kutoka kwa Mungu je hatutapokea maovu pia? (Ayubu 2:10). Na tena mwandishi aliyevuviwa wa kitabu (kama vile alivyofanya katika 1:22) anampongeza Ayubu kwa kusema, “Katika hayo yote Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake.”

 

Kwa maneno mengine: Huu ni mtazamo sahihi wa ukuu wa Mungu juu ya Shetani. Shetani ni halisi na anaweza kuwa na mkono katika misiba yetu, lakini sio mkono wa mwisho, na sio mkono wa maamuzi. 


Yakobo anaweka wazi kwamba Mungu alikuwa na kusudi zuri katika mateso yote ya Ayubu:


“Mmesikia habari za uthabiti wa Ayubu, na kuyaona makusudi ya Bwana, jinsi Bwana alivyo na huruma na rehema” (Yakobo 5:11).

 

Kwa hiyo, ingawa Shetani alihusika, kusudi kuu lilikuwa la Mungu, nalo lilikuwa “lenye huruma na rehema.”

 

Hili ndilo somo lilelile tunalojifunza katika 2 Wakorintho 12:7 , ambapo Paulo asema kwamba mwiba wake katika mwili ulikuwa “mjumbe wa Shetani” na bado ulitolewa kwa kusudi la utakatifu wake mwenyewe— ili kumzuia asijivune . “Kwa ajili ya ukuu wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani, ili kunisumbua, ili nisiwe na kiburi.

 

Sasa, unyenyekevu sio kusudi la Shetani katika dhiki hii. Kwa hiyo, kusudi ni la Mungu. Maana yake ni kwamba hapa Shetani anatumiwa na Mungu kutimiza makusudi yake mema katika maisha ya Paulo. Kwa hakika, kwa wana wateule wa Mungu, Shetani hawezi kutuangamiza, na Mungu anageuza mashambulizi yake yote hatimaye dhidi yake na kwa ajili yetu.

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page