top of page

Jinsi Tunavyopaswa Kupigania Utakatifu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • May 29
  • 2 min read
ree

Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao. (Waebrania 12:14)

 

Kuna utakatifu wa kimatendo ambao bila yake hatutamwona Bwana. Wengi wanaishi kana kwamba haikuwa hivyo.

 

Kuna wanaojiita Wakristo ambao wanaishi maisha machafu kiasi kwamba watasikia maneno ya Yesu ya kutisha, “Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu” (Mathayo 7:23). Paulo anasema kwa wanaodai kuwa waamini, “Kama mkiishi kufuatana na mwili, mtakufa” (Warumi 8:13).

 

Kwa hiyo,

kuna utakatifu ambao bila yake hakuna mtu atakayemwona Bwana. Na kujifunza kupigania utakatifu kwa imani katika neema ya wakati ujao ni muhimu sana. 

 

Kuna njia nyingine ya kufuata utakatifu ambayo inarudisha nyuma na kusababisha kifo. Paulo anatuonya dhidi ya kumtumikia Mungu kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kwa imani katika neema yake inayowezesha. Mungu "hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji chochote, kwa kuwa yeye mwenyewe huwapa watu wote uzima na pumzi na kila kitu" (Matendo 17:25). Jitihada zozote za kumtumikia Mungu ambazo, kwa tendo hilohilo, hazimtegemei yeye kuwa thawabu ya mioyo yetu na nguvu za utumishi wetu, zitamvunjia heshima kama mungu wa kipagani mwenye uhitaji.

 

Petro anafafanua njia mbadala ya utumishi huo wa kujitegemea wa Mungu, “Yeyote anayetumikia, [na afanye hivyo] kama mtumishi kwa nguvu anazojaliwa na Mungu, ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kupitia Yesu Kristo” (1 Petro. 4:11). Na Paulo asema, “Sitathubutu kunena neno lo lote isipokuwa yale ambayo Kristo ametimiza kupitia mimi” (Warumi 15:18; tazama pia 1 Wakorintho 15:10). 

 

Muda baada ya muda, neema inafika ili kutuwezesha kufanya “kila kazi njema” ambayo Mungu ametuwekea. “Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema” (2 Wakorintho 9:8). 

 

Mapambano ya matendo mema ni mapambano ya kuamini ahadi za neema ya wakati ujao.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page