top of page

Jinsi ya Kuchukia Maisha Yako

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 2 min read

Updated: May 1

ree

“Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika ardhi na kufa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; lakini ikifa, hutoa matunda mengi.  Yeyote anayeyapenda maisha yake atayapoteza, na yeyote anayeyachukia maisha yake katika ulimwengu huu atayaweka hata uzima wa milele." (Yohana 12:24-25)

 

"Yeyote anayechukia maisha yake katika ulimwengu huu atayaweka hata uzima wa milele." Hii ina maana gani?

 

Inamaanisha, angalau, kwamba usifikiri sana juu ya maisha yako katika ulimwengu huu. Kwa maneno mengine, haijalishi sana nini kitakachotokea kwenye maisha yako katika ulimwengu huu.

 

Ikiwa watu watazungumza vizuri juu yako, haijalishi sana.

Ikiwa wanakuchukia, haijalishi sana.

Ikiwa una vitu vingi, haijalishi sana.

Ikiwa unayo kidogo, haijalishi sana.

Ikiwa unateswa au kusingiziwa uongo, haijalishi sana.

Ikiwa wewe ni maarufu au haujulikani, haijalishi sana.

Ikiwa umekufa pamoja na Kristo, mambo haya hayajalishi sana.

 

Lakini maneno ya Yesu ni makali zaidi. Yesu anatuita sio tu kuvumilia uzoefu ambao hatujauchagua, lakini kufanya uchaguzi wa kumfuata. "Mtu akinitumikia, lazima anifuate" (Yohana 12:26). Unakwenda wapi? Anasogea katika Gethsemane na kuelekea msalabani.


Yesu hasemi tu: Ikiwa mambo yakiharibika, usifadhaike, kwa kuwa hata hivyo umekufa pamoja nami. Anasema: Chagua kufa pamoja nami. Chagua kuchukia maisha yako katika ulimwengu huu jinsi nilivyochagua msalaba.

 

Hiki ndicho Yesu alimaanisha aliposema, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate” (Mathayo 16:24). Anatuita ili tuuchague msalaba. Watu walifanya jambo moja tu msalabani. Walikufa juu yake. “Jitwike msalaba wako,” maana yake, “Kama chembe ya ngano, anguka ardhini na ufe.” Chagua kufa.

 

Lakini kwanini? Kwa ajili ya dhamira kali kwa huduma: “ Siuhesabu uhai wangu kuwa kitu chochote wala si kitu cha thamani kwangu mwenyewe , ikiwa tu nitaumaliza mwendo wangu na huduma niliyopokea kwa Bwana Yesu ya kutangazia Injili ya neema ya Mungu” (Matendo 20:24). Nafikiri ninamsikia Paulo akisema, “Haijalishi nini kinanipata —iwapo tu kama ninaweza kuishi kwa ajili ya utukufu wa neema ya Mungu.”

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page