top of page

Jinsi ya Kujibu Unapokosea

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Mar 31
  • 1 min read

Kwa maana lile jema nilipendalo silitendi, bali lile baya nisilolipenda ndilo ninaloendelea kufanya. (Warumi 7:19)


Wakristo hawaishi katika kushindwa tu. Lakini pia hatuishi tu katika ushindi mkamilifu dhidi ya dhambi. Na katika nyakati za kushindwa dhidi ya dhambi, Warumi 7:13–25 inatuonyesha njia ya kawaida ambayo Mkristo mwenye afya anapaswa kuitikia.

 

Tunapaswa kusema:

  1. Naipenda sheria ya Mungu. (mstari wa 22)

  2. Ninachukia nilichotoka kufanya. (mstari wa 15)

  3. Mimi ni mtu mnyonge! Ni nani atakayeniweka huru kutoka katika mwili wa kifo hiki? (mstari wa 24)

  4. Asante Mungu! Ushindi utakuja kwa Yesu Kristo Bwana wangu. (mstari wa 25)

 

Kwa maneno mengine, hakuna Mkristo anayetaka kuishi katika kushindwa. Hakuna Mkristo anayekubali kuishi katika kushindwa. Lakini tukishindwa kwa muda, hatupaswi kusema uwongo juu ya hilo.

 

Hakuna unafiki. Hakuna kujifanya. Hakuna ukamilifu wa kujivunia Hakuna tabasamu bandia au furaha ya juu juu.

 

Na zaidi ya yote, Mungu tuepushe na upofu wa kushindwa kwetu wenyewe na haraka ya kuwahukumu wengine.

 

Mungu, tusaidie kuhisi vibaya zaidi kuhusu mapungufu yetu wenyewe kuliko kushindwa kwa wengine.


Mungu, tupe uaminifu, unyoofu, na unyenyekevu wa mtume Paulo katika maandiko haya! “Mtu mnyonge mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Ashukuriwe Mungu katika Yesu Kristo Bwana wetu! (Warumi 7:24-25).

Comentarios


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page