top of page

Jinsi ya Kumtukuza Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Nov 14
  • 1 min read
ree

Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo; nitamtukuza kwa shukrani. (Zaburi 69:30)

 

Kuna aina mbili za ukuzaji: ukuzaji wa hadubini na ukuzaji wa darubini. Moja anafanya kitu kidogo kionekane kikubwa kuliko kilivyo. Nyingine hufanya kitu kikubwa kuonekana kwa ukubwa wake kweli.

 

Daudi anaposema, “Nitamtukuza Mungu kwa shukrani,” hamaanishi, “nitamfanya Mungu mdogo aonekane mkubwa kuliko alivyo.” Anamaanisha, “Nitamfanya Mungu mkubwa aanze kuonekana kuwa mkubwa kama alivyo.”

 

Hatujaitwa kuwa hadubini. Tumeitwa kuwa darubini. Wakristo hawajaitwa kuwa walaghai ambao wanakuza bidhaa zao kutoka kwenye uwiano wote wa hali halisi, wakati wanajua bidhaa ya mshindani ni bora zaidi. Hakuna kitu na hakuna aliye mkuu kuliko Mungu. Na hivyo wito wa wale wanaompenda Mungu ni kufanya ukuu wake uanze kuonekana mkuu jinsi ulivyo. 

 

Hiyo ndio sababu ya uwepo wetu, ndiyo maana tuliokolewa, kama Petro asemavyo katika 1 Petro 2:9, “Ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki yake mwenyewe, mpate kuzitangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.”

 

Wajibu wote wa Mkristo unaweza kufupishwa katika hili: kuhisi, kufikiri, na kutenda kwa njia ambayo itamfanya Mungu aonekane mkuu jinsi alivyo.

Kuwa darubini kwa ajili ya ulimwengu uone utajiri usio na kikomo wa utukufu wa Mungu.

 

Hii ndiyo maana ya Mkristo kumtukuza Mungu. Lakini huwezi kukuza kile ambacho hujakiona au unachosahau haraka.

 

Kwa hiyo, kazi yetu ya kwanza ni kuona na kukumbuka ukuu na wema wa Mungu. Kwa hiyo tunasali kwa Mungu, “Fungua macho ya moyo wangu!” (Waefeso 1:18), na tunahubiria nafsi zetu, “Nafsi, usisahau fadhili zake zote!” (Zaburi 103:2).

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page