Jinsi ya Kuomba Msamaha
- Dalvin Mwamakula
- Apr 28
- 2 min read
Updated: May 1

Yeye ni mwaminifu na wa haki, ata tusamehe dhambi zetu. (1 Yohana 1:9)
Ninakumbuka nilipomsikia mmoja wa maprofesa wangu katika seminari akisema kwamba mojawapo ya majaribio bora zaidi ya theolojia ya mtu ilikuwa ni athari iliyonayo kwenye maombi yetu.
Hili lilinigusa kama ukweli kwa sababu ya kile kilichokuwa kikitokea katika maisha yangu. Mimi na Noël tulikuwa tumefunga ndoa tu na tulikuwa tukiendelea na tabia yetu ya kusali pamoja kila jioni. Niliona kwamba wakati wa kozi za Biblia ambazo zilikuwa zikiunda theolojia yangu kwa undani zaidi, maombi yangu yalianza kubadilika ghafla.
Pengine badiliko la maana zaidi katika siku hizo lilikuwa kwamba nilikuwa nikijifunza kutoa hoja yangu mbele za Mungu kutokana na msingi wa utukufu wake. Kuanzia na “ Jina lako litukuzwe ” na kumalizia na “Katika jina la Yesu ” kulimaanisha kwamba utukufu wa jina la Mungu ulikuwa lengo na msingi wa kila kitu nilichoomba.
Na ni nguvu kubwa kiasi gani iliyoingia maishani mwangu nilipojifunza kwamba kuomba msamaha hakupaswi kutegemea tu huruma ya Mungu, bali pia haki yake katika kuhesabu thamani ya utii wa Mwanawe.
Mungu ni mwaminifu na mwenye haki, naye atakusamehe dhambi zako. (1 Yohana 1:9).
Katika Agano Jipya, msingi wa msamaha wote wa dhambi umefunuliwa wazi zaidi kuliko ilivyokuwa katika Agano la Kale, lakini msingi wakujitolea kwa Mungu kwa ajili ya jina lake, haubadiliki.
Paulo anafundisha kwamba kifo cha Kristo kilidhihirisha haki ya Mungu kwa kutokuzingatia dhambi, na kuthibitisha haki ya Mungu katika kuwahesabia haki wasiomcha Mungu wanaomtegemea Yesu na sio wao wenyewe (Warumi 3:25-26).
Kwa maneno mengine, Kristo alikufa mara moja tu kwa wakati wote ili kuitakasa sifa ya Mungu kutokana na kile kinachoonekana kama upotoshaji mkubwa wa haki—kuwaachilia huru wenye dhambi wenye hatia kwa sababu tu ya Yesu. Lakini Yesu alikufa kwa namna ambayo msamaha “kwa ajili ya Yesu” ni sawa na msamaha “kwa ajili ya jina la Mungu.” Hivyo basi, hakuna upotoshaji wa haki. Jina la Mungu, haki yake na uadilifu wake, vinathibitishwa na kutukuzwa katika tendo lile lile la kutoa dhabihu hiyo yenye kumheshimu Mungu.
Kama Yesu alivyosema alipoikabili saa ile ya mwisho, “Sasa roho yangu inafadhaika. Na niseme nini? 'Baba, niokoe kutokana na saa hii'? Lakini kwa kusudi hili nimekuja saa hii. Baba, ulitukuze jina lako” (Yohana 12:27–28). Hivyo ndivyo alivyofanya—ili awe mwenye haki na mwenye kuwahesabia haki wale wanaomtumaini Yesu (Warumi 3:26).




Comments