top of page

Jinsi ya Kupambana na Wasiwasi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 2
  • 2 min read
ree

[Mtwikeni] mahangaiko yenu yote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. (1 Petro 5:7)


Zaburi 56:3 inasema, “Ninapoogopa, ninaweka tumaini langu kwako.”


Angalia: haisemi, "Sipambani na hofu." Hofu inakuja, na vita huanza. Kwa hiyo Biblia haidhani kwamba waamini wa kweli hawatakuwa na wasiwasi. Badala yake, Biblia hutuambia jinsi ya kupigana unapotushambulia.


Kwa mfano, andiko la 1 Petro 5:7 linasema, “[Mtupe] mahangaiko yenu yote juu yake, kwa sababu yeye anawajali ninyi.” Haisemi, hutawahi kuhisi wasiwasi wowote. Inasema, ukiwa nao, mtupie Mungu. Wakati matope yanapotapakaa kwenye kioo cha mbele na unapoteza kwa muda kuona barabara na kuanza kuyumba kwa wasiwasi, washa vipangusio na nyunyiza maji ya kuosha kioo.


Kwa hivyo jibu langu kwa mtu ambaye anapaswa kukabiliana na hisia za wasiwasi kila siku ni kusema: hiyo ni hali ya kawaida. Angalau imekuwa hivyo kwa upande wangu, tangu miaka yangu ya ujana. Suala ni: Je, tunapambanaje nao?


Jibu la swali hilo ni:


Tunapambana na mahangaiko kwa kupigana na kutokuamini na kupigania imani katika neema ya wakati ujao.

Na jinsi unavyopigana hivi “vita vilivyo vizuri” (1 Timotheo 6:12; 2 Timotheo 4:7) ni kwa kutafakari juu ya uhakikisho wa Mungu wa neema ya wakati ujao na kwa kuomba msaada wa Roho wake.


Vipangusio vya kioo ni ahadi za Mungu zinazofuta matope ya kutokuamini, na maji ya kuosha kioo ni msaada wa Roho Mtakatifu. Vita ya kuwa huru kutoka katika dhambi - ikiwa ni pamoja na dhambi ya wasiwasi - inapiganwa "na Roho na imani katika ukweli" (2 Wathesalonike 2:13).


Kazi ya Roho na neno la kweli. Hawa ndio wajenzi wakubwa wa imani. Bila kazi ya kulainisha ya Roho Mtakatifu, vipangusio vya neno hujikwaruza tu juu ya matope yanayopofusha ya kutoamini kwenye kioo cha mbele.


Vyote viwili ni muhimu: Roho na neno. Tunasoma ahadi za Mungu na tunaomba msaada wa Roho wake. Na kioo cha mbele kinaposafishwa ili tuweze kuona hali njema ambayo Mungu anatupangia (Yeremia 29:11), imani yetu huimarika na kuyumba yumba kwa wasiwasi kunaondoka.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page