top of page

Jinsi ya Kupinga Tamaa ya Dhambi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jun 30
  • 2 min read
ree

Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao; akachaguwa kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha kwa anasa za dhambi za muda mfupi.  Aliona kushutumiwa kwake  kwa ajili ya Kristo ni utajiri mkubwa kuliko hazina za Misri, maana alikuwa anatazamia kupata thawabu baadaye. (Waebrania 11:24-26)


Au, tufikirie mambo ya lazima tu: “Kwa imani Musa . . . [aliacha] kujifurahisha kwa anasa za dhambi za muda mfupi . . . kwa maana alikuwa anatazamia kupata thawabu” (Waebrania 11:24–26).


Imani haitosheki na “anasa za haraka.” Ina njaa kubwa kwa ajili ya furaha. Furaha inayodumu. Milele.

Na neno la Mungu linasema, “Mbele za uso wako kuna furaha tele; kwenye mkono wako wa kuume kuna mema ya milele” (Zaburi 16:11). Kwa hiyo, imani haitakengeushwa na kuingia katika raha za udanganyifu za dhambi. Haitakata tamaa kirahisi hivyo katika utafutaji wake wa furaha kuu na kamili.

Jukumu la neno la Mungu ni kuilisha hamu ya imani kwa ajili ya Mungu. Na, kwa kufanya hivi, kunaondoa moyo wangu kwenye ladha ya udanganyifu ya tamaa.


Tamaa ilianza kunihadaa kuhisi kwamba ningekosa kuridhika sana ikiwa ningefuata njia ya usafi. Lakini basi ninachukua upanga wa Roho na kuanza kupigana.


  • Nilisoma kwamba ni afadhali kuling'oa jicho langu kuliko kutamani (Mathayo 5:29).


  • Nilisoma kwamba nikifikiri juu ya mambo yaliyo safi na ya kupendeza na bora, amani ya Mungu itakuwa pamoja nami (Wafilipi 4:8–9).


  • Nilisoma kwamba kuweka nia katika mwili huleta kifo, lakini kuweka nia katika Roho huleta uzima na amani (Warumi 8: 6).


  • Nilisoma kwamba tamaa hufanya vita dhidi ya nafsi yangu (1 Petro 2:11), na kwamba raha za maisha haya husonga uzima wa Roho (Luka 8:14).


  • Lakini bora zaidi, nilisoma kwamba Mungu hawanyimi vitu vizuri wale wanaotembea kwa unyoofu (Zaburi 84:11), na kwamba walio safi moyoni watamwona Mungu (Mathayo 5:8).


Ninaposali ili imani yangu itosheke na maisha na amani ya Mungu, upanga wa Roho uliondoa sukari iliyo pakwa juu ya sumu ya tamaa. Ninaiona kama ilivyo. Na kwa neema ya Mungu, nguvu zake za kuvutia zimevunjwa.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page