top of page

Kosa la Kuogopa Mwanadamu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • May 29
  • 1 min read
ree

Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi, kwa kuwa nimeihalifu amri ya Bwana, na maneno yako, kwa sababu niliwaogopa watu na kutii sauti yao. (1 Samweli 15:24)


Kwa nini Sauli alitii watu badala ya Mungu? Kwa sababu aliwaogopa watu badala ya Mwenyezi Mungu. Aliogopa matokeo ya wanadamu ya utii zaidi kuliko kuogopa matokeo ya kimungu ya kutokutii. Aliogopa kutofurahishwa kwa watu zaidi kuliko kutofurahishwa na Mungu. Na hilo ni tusi kubwa kwa Mungu. 


Kwa hakika, Isaya anasema ni aina ya kiburi kuogopa kile ambacho mwanadamu anaweza kufanya huku tukipuuza ahadi za Mungu. Anamnukuu Mungu kwa swali hili linalo choma: “Mimi, mimi, ndimi niwafarijiye ninyi; wewe ni nani hata umwogope mwanadamu afaye, na mwanadamu aliyefanywa kama majani, na kumsahau Bwana, Muumba wako? (Isaya 51:12–13). 


Kumwogopa mwanadamu kunaweza kusionekane kama kiburi, lakini ndivyo Mungu asemavyo,

“Unafikiri wewe ni nani kumwogopa mwanadamu na kunisahau mimi Muumba wako!”

Jambo kuu ni hili: Ikiwa unamwogopa mwanadamu, umeanza kukataa utakatifu, thamani ya Mungu na Mwanawe, Yesu. Mungu ana nguvu isiyo na mwisho kuliko mwanadamu. Yeye ni mwenye hekima isiyo na mwisho na amejaa thawabu na furaha isiyo na mwisho. 


Kumwacha kwa kuogopa kile ambacho mwanadamu anaweza kufanya ni kupunguza yale yote ambayo Mungu anaahidi kuwa kwa wale wanaomcha. Ni dharau kubwa. Na katika dharau kama hizi Mungu hawezi kufurahishwa. 


Kwa upande mwingine, tunaposikia ahadi za Mungu na kumtumaini kwa ujasiri, tukiogopa lawama inayoletwa juu ya Mungu kwa kutokuamini kwetu, basi anaheshimiwa sana. Na katika hilo ana furaha nyingi.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page