top of page

Kristo kama Njia na Hatima

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jan 27
  • 2 min read
ree

Nimesulubishwa pamoja na Kristo. Si mimi tena ninayeishi, bali Kristo anaishi ndani yangu. Na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda na kujitoa nafsi yake kwa ajili yangu. (Wagalatia 2:20)

 

Kwanini Mungu aliumba ulimwengu? Na kwa nini anautawala kwa namna hii? Mungu anafanikisha nini? Je, Yesu Kristo ni njia ya mafanikio haya au lengo la mafanikio?

 

Yesu Kristo ndiye ufunuo mkuu wa Mungu. Yeye ni Mungu katika umbo la mwanadamu. Kwa hivyo, yeye ndiye mwisho, sio njia. 

 

Udhihirisho wa utukufu wa Mungu ndio maana ya ulimwengu. Hiki ndicho Mungu anafanikisha. Mbingu, na historia ya ulimwengu, “vinatangaza utukufu wa Mungu.” 

 

Lakini Yesu Kristo alitumwa kutimiza jambo fulani lililohitaji kufanywa. Alikuja kurekebisha anguko. Alikuja kuwaokoa wenye dhambi kutokana na uharibifu usioepukika kwa sababu ya dhambi zao. Waliokombolewa hawa wataona, kufurahia, na kuonyesha utukufu wa Mungu kwa furaha ya milele.

 

Wengine wataendelea kurundika dharau juu ya utukufu wa Mungu. Kwa hiyo, Yesu Kristo ndiye njia ambayo Mungu alikusudia kufanikisha katika kuonyesha utukufu wake kwa ajili ya furaha ya watu wake. Hakuna mtu ambaye angeona na kufurahia na kusherehekea utukufu wa Mungu mbali na kazi ya wokovu ya Kristo. Kusudi la ulimwengu lingeisha. Kwahiyo, Kristo ni njia.


Yesu ndiye hatima ambayo ulimwengu ulifanywa kwa ajili yake, na ndiye njia inayowezesha kusudi hilo kufurahiwa na wenye dhambi waliohesabiwa haki.

 

Lakini katika utimilifu huo msalabani, alipokufa kwa ajili ya wenye dhambi, Kristo alidhihirisha upendo na haki ya Baba kwa njia kuu. Hiki kilikuwa kilele cha ufunuo wa utukufu wa Mungu — utukufu wa neema yake.

 

Kwa hiyo, wakati wa tendo lake kamilifu akiwa njia ya kusudi la Mungu, Yesu akawa mwisho wa kusudi hilo. Alikufa kwa ajili ya wenye dhambi na kufufuka kwa ajili ya maisha yao, akawa ufunuo mkuu na wa juu zaidi wa utukufu wa Mungu.

 

Kwa hiyo Kristo aliyesulubiwa ndiye njia na mwisho wa kusudi la Mungu katika ulimwengu. 

Bila kazi yake, mwisho huo — kufunua utimilifu wa utukufu wa Mungu kwa furaha ya watu wa Mungu — usingetokea. 

 

Na katika kazi hiyohiyo akawa mwisho — yule ambaye milele na milele atakuwa lengo la ibada yetu tunapotumia umilele kuona na kufurahia zaidi na zaidi yale aliyofunua juu ya Mungu alipofanyika laana kwa ajili yetu. 

 

Yesu ndiye mwisho ambao ulimwengu ulifanywa kwa ajili yake, na ndiye njia inayowezesha kusudi hilo kufurahiwa na wenye dhambi waliohesabiwa haki.


Yesu Kristo ni ufunuo mkuu wa Mungu, na njia ya kufurahia utukufu wa Mungu kupitia wokovu. Bila Kristo, kusudi la ulimwengu lingeisha.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page