top of page

Kristo ni kama Mwanga wa Jua

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 15
  • 2 min read
ree

Yeye ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na chapa halisi ya asili yake. (Waebrania 1:3)

 

Yesu uhusiana na mungu namna ambavyo mng'ao uhusiana na utukufu,  au namna ambavyo miali ya jua uhusiana na jua. 

 

Kumbuka kwamba kila mfano kati ya Mungu na vitu vya asili si mkamilifu na utapotosha ukisisitiza sana. Hata hivyo, fikiria kwa mfano,

 

  1. Hakuna wakati ambapo jua lipo bila miale ya mwanga. Haviwezi kutenganishwa. Mwangaza ni wa milele pamoja na utukufu. Kristo ni wa milele pamoja na Mungu Baba.

  2. Mwangaza ni utukufu unaong’aa nje. Si tofauti sana na utukufu. Kristo ni Mungu anayesimama kama yupo tofauti lakini si tofauti kimsingi na Baba.

  3. Hivyo mwanga unazaliwa milele, kama vile, na utukufu — haukuumbwa au kutengenezwa. Ukiweka kikokotozi kinachoendeshwa na jua kwenye mwanga wa jua, namba zinaonekana kwenye uso wa kikokotozi. Hizi, unaweza kusema, zimeumbwa au kufanywa na jua, lakini siyo jua lenyewe. Lakini miale ya jua ni mwendelezo wa jua. Kwa hivyo Kristo amezaliwa milele na Baba, lakini hakuumbwa wala kufanywa.

  4. Tunaona jua kwa njia ya kuona miale ya jua. Kwa hivyo tunamwona Mungu Baba kwa kumwona Yesu. Miale ya jua hufika hapa takriban dakika nane baada ya kuondoka kwenye jua, na mpira wa moto unaoonekana angani ni taswira — mwakilishi halisi — wa jua; si kwa sababu ni picha ya jua, bali kwa sababu ni jua linaloangaza kwa mng’ao wake.

 

Kwa hivyo nampendekeza mtu huyu mkuu kwako ili uweze kumwamini, kumpenda, na kumwabudu. Yeye yuko hai na ameketi mkono wa kuume wa Mungu akiwa na nguvu na mamlaka yote na siku moja atakuja kwa utukufu mkuu. Ana nafasi hiyo ya juu kwa sababu yeye mwenyewe ni Mungu Mwana, “mng’ao wa utukufu wa Mungu na chapa halisi ya asili yake.”

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page