Kuabudu Katika Dhoruba ya Radi
- Dalvin Mwamakula
- Sep 2
- 1 min read

“Kwa maana kama vile radi imulikavyo katika anga kuanzia mwisho mmoja hadi mwingine, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake” (Luka 17:24)
Nilisafiri kwa ndege usiku kutoka Chicago hadi Minneapolis, kama vile peke yangu kwenye ndege. Rubani alitangaza kwamba kulikuwa na radi kwenye Ziwa Michigan na kuelekea Wisconsin. Angeliizungusha upande wa magharibi ili kuepuka msukosuko.
Nikiwa nimekaa pale nikitazama nje kwenye weusi kabisa upande wa mashariki wa ndege, ghafla anga yote ikang'aa kwa mwanga, na pango la mawingu meupe likaanguka maili nne chini ya ndege na kisha kutoweka.
Sekunde moja baadaye, handaki kubwa jeupe la mwanga lililipuka kutoka kaskazini hadi kusini kuvuka upeo wa macho, na likatoweka tena na kuwa nyeusi. Hivi karibuni radi zilitokea kila wakati, na volkeno za nuru zilipasuka kutoka kwenye mifereji ya mawingu na kutoka nyuma ya milima ya mbali ya mawingu meupe.
Nilikaa huku nikitikisa kichwa karibu kwa kutoamini. Ee Bwana, ikiwa hizi ni cheche za unoaji wa upanga wako, itakuwaje siku ya kutokea kwako! Na nikakumbuka maneno ya Kristo: “Kwa maana kama vile radi imulikavyo katika anga kuanzia mwisho mmoja hadi mwingine, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake” (Luka 17:24).
Hata sasa ninapokumbuka maono hayo, neno utukufu linajaza hisia zangu.
Ninamshukuru Mungu kwamba tena na tena ameuamsha moyo wangu kumtamani, kumwona, na kuketi kwenye karamu ya Furaha ya Kikristo na kumwabudu Mfalme wa Utukufu.
Ukumbi wa karamu ni mkubwa sana. Njoo.




Comments