top of page

Kufurahia Kusifu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 2 min read
ree

Watu na wakusifu, Ee Mungu; watu wote na wakusifu! (Zaburi 67:35,5)

 

Kwanini Mungu anaamuru kwamba lazima tumsifu Mungu?

 

CS Lewis:


Kama vile watu wanavyosifu kwa hiari chochote wanachothamini, vivyo hivyo wanatuhimiza kwa hiari kujiunga nao katika kusifu: “Si ni mrembo? Si ilikuwa ya ajabu? Hujadhani kwamba hiyo ilikuwa ya kuvutia mno?”

 

Waandishi wa Zaburi, wanapowaambia wote wamsifu Mungu, wanafanya kile ambacho wanadamu wote hufanya wanapozungumza kuhusu kile wanachokithamini. Ugumu wangu mkubwa, wa jumla, kuhusu suala la kumsifu Mungu ulitegemea hoja ya kipuuzi ya kumnyima mwanadamu kile anachopenda kufanya kwa yale yote anayoyathamini, linapokuja kwa Yule aliye wa Thamani ya Juu kabisa.

 

Nadhani tunafurahia kusifu kile tunachokifurahia kwa sababu sifa haionyeshi tu furaha hiyo, bali huikamilisha; ni utimilifu uliokusudiwa. Wapenzi hawasifiani kwa sababu ya heshima tu; huendelea kuambiana jinsi walivyo wazuri kwa sababu furaha haijakamilika hadi itakaposemwa.

 

Hili ndio jibu - suluhu kwa kile kinachoonekana kuwa ubinafsi wa Mungu katika kudai sisi tumsifu! Ni hitaji la furaha yetu kuu. Tunasifu kile tunachofurahia kwa sababu furaha haijakamilika hadi inapoonyeshwa kwa sifa. Iwapo hatungeruhusiwa kuzungumza kuhusu tunachothamini na kusherehekea tunachopenda na kusifu tunachokipenda, furaha yetu isingekuwa kamili.

 

Hivyo basi, ikiwa Mungu anatupenda vya kutosha kutufanya tufurahie kikamilifu, haipaswi tu kujitoa mwenyewe kwetu; lazima pia ashinde kutoka kwetu sifa ya mioyo yetu — si kwa sababu anahitaji kuimarisha udhaifu fulani ndani yake au kufidia kasoro yoyote, bali kwa sababu anatupenda na anatafuta ukamilifu wa furaha yetu, furaha inayopatikana tu katika kumjua na kumsifu yeye, aliye mkuu kuliko viumbe vyote.

 

Ikiwa kweli yuko kwa ajili yetu, lazima awe kwa ajili yake mwenyewe! Mungu ndiye pekee katika ulimwengu wote ambaye kutafuta sifa zake mwenyewe ndilo tendo kuu la upendo. Kwake yeye, kujikweza ni sifa ya juu kabisa. Anapofanya mambo yote “kwa sifa ya utukufu wake” (Waefeso 1:12,14), anatuhifadhi na kutuzawadia kitu pekee katika ulimwengu wote ambacho kinaweza kuzitosheleza tamaa zetu.

 

Mungu yu upande wetu! Na msingi wa upendo huu ni kwamba Mungu amekuwa, yuko sasa, na atakuwa milele upande wake mwenyewe.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page