top of page

Kuridhika na Maagizo Yake

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 2 min read

Updated: May 1

Huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake. Na amri zake sio mzigo mzito. Kwa maana kila mtu aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, imani yetu. Ni nani anayeushinda ulimwengu isipokuwa ni yeye aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? (1 Yohana 5:3-5)


Kilicho wazi katika mistari hii ni kwamba kuzaliwa mara ya pili - kuzaliwa tena na Mungu - hugeuza amri za Mungu kutoka kuwa mzigo mzito na kuwa furaha yetu. Je, hilo linafanyaje kazi?

 

Je, ni kwa jinsi gani kuzaliwa na Mungu hufanya amri za Mungu kuwa furaha badala ya kuwa mzigo?

 

Mtume Yohana anasema, “Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, imani yetu” (1 Yohana 5:4). Kwa maneno mengine, jinsi kuzaliwa na Mungu kunashinda mzigo mzito wa kilimwengu juu ya amri za Mungu ni kwa kupata imani. Hilo linathibitishwa katika 1 Yohana 5:1, ambayo husema, kihalisi, “Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ndiye Kristo amezaliwa na Mungu.”

 

Imani ni uthibitisho kwamba tumezaliwa na Mungu. Hatujisababishi sisi wenyewe kuzaliwa mara ya pili kwa kuamua kuamini. Mungu huumba utayari wetu wa kuamini kwa kutufanya sisi kuzaliwa mara ya pili. Kama vile Petro alivyosema katika barua yake ya kwanza, Mungu “alitusababisha sisi kuzaliwa mara ya pili kwa tumaini lililo hai” (1 Petro 1:3). Tumaini letu lililo hai, au imani katika neema ya wakati ujao, ni kazi ya Mungu kupitia kuzaliwa upya.

 

Imani inayoshinda uadui wetu kwa Mungu hutuweka huru kuzishika amri zake na kusema kama mtunga-zaburi, “Kufanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu.”

Kwa hiyo, Yohana anaposema, “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu,” na kisha kuongeza, “Na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, imani yetu ” (1 Yohana 5:4), ninamwelewa kumaanisha kwamba Mungu hutuwezesha, kwa kuzaliwa upya, kuushinda ulimwengu—yaani, kuushinda utovu wetu wa kidunia wa kushika amri za Mungu. Kuzaliwa upya hufanya hivyo kwa kusitawisha imani, ambayo kwa wazi inahusisha mwelekeo wa kupendezwa na amri za Mungu, badala ya kukengeushwa na amri za Mungu, ili zihisi kuwa mzigo mzito.

 

Kwa hiyo, ni imani inayoshinda uadui wetu tuliozaliwa nao kwa Mungu na mapenzi yake, na hutuweka huru kuzishika amri zake na kusema pamoja na mtunga-zaburi, “Kufanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu” (Zaburi 40:8).


Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page