top of page

Kusamehewa kwa ajili ya Yesu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 2 min read
ree

Kwa ajili ya jina lako, ee Mwenyezi-Mungu, unisamehe kosa langu, maana ni kubwa. (Zaburi 25:11)

 

Katika kujua kilicho sahihi, Mungu hafuati mamlaka yoyote iliyo juu yake mwenyewe. Thamani yake mwenyewe ndio dhamana kuu katika ulimwengu. Kwa hiyo, kwa Mungu kufanya kilicho sahihi inamaanisha kutenda kwa njia inayolingana na thamani hii ya juu kabisa. 

 

Haki ya Mungu ni bidii isiyo na kipimo, furaha, na raha anayopata katika kile kilicho na thamani kuu, yaani, ukamilifu na thamani yake mwenyewe. Na kama angetenda kinyume na shauku hii ya milele kwa ukamilifu wake mwenyewe, atakuwa mdhalimu - angekuwa mwabudu sanamu.

 

Mungu mwenye haki kama huyo atawekaje upendo wake juu ya watenda-dhambi kama sisi ambao tumedharau ukamilifu wake? Lakini ajabu ya injili ni kwamba katika haki yake ya kimungu kuna msingi pia wa wokovu wetu.

 

Heshima isiyo na kikomo ambayo Baba anayo kwa Mwana hufanya iwezekane kwangu, mtenda dhambi mwovu, kupendwa na kukubalika ndani ya Mwana, kwa sababu katika kifo chake alithibitisha thamani na utukufu wa Baba yake.

Kwa sababu ya Kristo, tunaweza kuomba tukiwa na ufahamu mpya wa sala ya mtunga-zaburi, “Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, unisamehe kosa langu, kwa kuwa ni kubwa” (Zaburi 25:11). Ufahamu mpya ni kwamba, kwa sababu ya Kristo, badala ya kuomba tu, “Kwa ajili ya jina lako, unisamehe hatia yangu,” sasa tunaomba, “Kwa ajili ya jina la Yesu, Ee Mungu, unisamehe hatia yangu.” 

 

Andiko la 1 Yohana 2:12 linasema, “Ninawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu kwa ajili ya jina lake,” likimlenga Yesu. Sasa Yesu amefanya upatanisho kwa ajili ya dhambi na kutetea heshima ya Baba ili ‘dhambi zetu zisamehewe kwa ajili ya jina lake .

 

Mungu ni mwenye haki. Hafichi dhambi chini ya zulia. Ikiwa mwenye dhambi ataachiliwa huru, mtu fulani hufa ili kuthibitisha thamani isiyo na kikomo ya utukufu wa Mungu ambayo mwenye dhambi aliichafua. Hivyo ndivyo Kristo alivyofanya. Kwa hiyo, “Kwa ajili ya jina lako, Ee Bwana” na “Kwa ajili ya jina la Yesu” ni sawa. Na ndio maana tunaomba kwa ujasiri ili tupate msamaha.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page