top of page

Kusudi La Kuumbwa Kwetu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 1 min read
ree

Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. (1 Petro 3:18)


Jambo kuu zaidi la habari njema — injili — ni kufurahia ushirika na Mungu mwenyewe. Hili linawekwa wazi hapa katika 1 Petro 3:18 katika maneno “ili atulete kwa Mungu.” Ndiyo maana Yesu alikufa.

 

Karama nyingine zote za injili zipo ili kufanya hili liwezekane. 

 

  • Tumesamehewa ili hatia yetu isituweke mbali na Mungu. 

  • Tunahesabiwa haki ili hukumu yetu isituweke mbali na Mungu. 

  • Mungu anapatanishwa ili ghadhabu yake isisimame kati yetu na Mungu kama Baba yetu.

  • Tumepewa uzima wa milele sasa, tukiwa na miili mipya katika ufufuo, ili tuwe na uwezo wa kuwa pamoja na Mungu milele na kumfurahia Mungu kikamilifu. 

 

Jaribu moyo wako. Kwanini unataka msamaha? Kwanini unataka kuhesabiwa haki? Kwanini unataka ghadhabu ya Mungu ipatanishwe? Kwanini unataka uzima wa milele?


Je, jibu la hakika ni, “Kwa sababu ninataka kumfurahia Mungu sasa na milele”?

 

Upendo wa injili ambao Mungu anatoa ni zawadi yake mwenyewe. Hiki ndicho tulichoumbiwa. Hiki ndicho tulichopoteza kwa sababu ya dhambi zetu. Hiki ndicho Kristo alichokuja kurejesha. 

 

“Mbele ya uwepo wako kuna furaha tele; mkono wako wa kuume kuna mema ya milele” (Zaburi 16:11).

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page