top of page

Kusudi la Mafanikio

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 7
  • 2 min read
ree

Mwivi asiibe tena, bali afadhali afanye bidii, akifanya kazi iliyo njema kwa mikono yake mwenyewe, ili apate kuwa na kitu cha kumgawia mtu aliye na uhitaji. (Waefeso 4:28)


Kuna viwango vitatu vya jinsi ya kuishi na vitu vya kimwili: (1) unaweza kuiba ili kuvipata; (2) au unaweza kufanya kazi ili kuvipata; (3) au unaweza kufanya kazi ili kuvipata ili uweze kuvitoa.

 

Wengi sana wanaojiita Wakristo wanaishi katika ngazi ya pili. Tunatukuza kazi dhidi ya wizi na kuombaomba, na tunahisi tumetenda kwa uadilifu ikiwa tumekataa wizi na kuombaomba, na kujitolea kwa kazi ya uaminifu kwa malipo ya siku. Hilo si jambo baya. Kazi ni bora kuliko kuiba na kuombaomba. Lakini hivyo sivyo mtume anavyotuitia.

 

Karibu nguvu zote za utamaduni wetu zinatuhimiza kuishi kwenye kiwango cha pili: kufanya kazi ili kupata. Lakini Biblia inatusukuma bila kuchoka hadi kwenye kiwango cha tatu: fanya kazi ili kupata ili kutoa. “Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema” (2 Wakorintho 9:8).

 

Viwanda vikubwa na mishahara mikubwa ni ukweli wa nyakati zetu, na si lazima iwe mbaya. Ubaya ni kudhani kwamba mshahara mkubwa lazima uambatane na maisha ya kifahari.

Kwa nini Mungu anatubariki kwa wingi? Ili tuwe na vya kutosha kuishi, na kisha kutumia kilichobaki kwa kazi zote nzuri zinazopunguza mateso ya kiroho na kimwili - mateso ya muda na ya milele. Vyakutosha kwa ajili yetu; ziada kwa ajili ya wengine.


Suala sio kiasi gani cha fedha mtu anachopata. Viwanda vikubwa na mishahara mikubwa ni ukweli wa nyakati zetu, na si lazima iwe mbaya. Ubaya upo katika kudanganywa na kufikiri kwamba mshahara mkubwa lazima uambatane na maisha ya kifahari.

 

Mungu ametufanya kuwa mikondo ya neema yake. Hatari iko katika kufikiria kuwa mkondo unapaswa kupambwa kwa dhahabu. Haitakiwi. Shaba itatosha. Shaba inaweza kubeba utajiri usio dhaniwa kwa wengine. Na katika mchakato wenyewe wa utoaji huo tunafurahia baraka kuu zaidi (Matendo 20:35).

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page