Kutosheka Milele
- Dalvin Mwamakula
- Feb 26
- 1 min read

"Mimi ni mkate wa uzima; yeyote anayekuja kwangu hataona njaa, na yeyote anayeamini mimi hataona kiu kamwe." (Yohana 6:35)
Maandishi haya yanaonyesha kwamba kumwamini Yesu ni kula na kunywa kutoka katika yote ambayo Yesu alivyo. Inaenda mbali zaidi na kusema kwamba kiu ya roho zetu inatoshelezwa na Yesu, ili tusione tena kiu.
Yeye ndiye mwisho wa safari yetu ya kutosheka. Hakuna kitu zaidi, na hakuna kilicho bora zaidi.
Tunapo mwamini Yesu kama Yohana anavyokusudia, uwepo na ahadi ya Yesu inatosheleza sana kiasi kwamba hatutawaliwi na vishawishi vya dhambi (angalia Warumi 6:14). Hii inaeleza ni kwanini imani kama hiyo kwa Yesu inabatilisha nguvu ya dhambi na kuwezesha utii.
Yesu ndiye mwisho wa safari yetu ya kutosheka. Kwa imani, Kristo ndani yetu ni chemchemi ya maisha yanayotosheleza, akituweka huru kutoka udanganyifu wa dhambi na kutuongoza mbinguni.
Yohana 4:14 inaelekeza katika mwelekeo huo huo: “Yeyote atakaye kunywa maji nitakayompa hataona kiu tena. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji inayobubujika hadi uzima wa milele." Kulingana na Yohana 6:35, imani ya wokovu inazungumziwa hapa kama kunywa maji yanayotosheleza tamaa za ndani kabisa za roho. Na utoshelevu huo unakuwa wenye tija, kama kisima kinachofurika.
Ni sawa katika Yohana 7:37-38: "Yesu alisimama na kupaza sauti, 'Kama mtu yeyote ana kiu, na aje kwangu anywe. Yeyote anayeamini ndani yangu, kama Maandiko yalivyosema, “Kutoka moyoni mwake itatiririka mito ya maji ya uzima.”
Kupitia imani, Kristo anakuwa ndani yetu chemchemi isiyokauka ya maisha yanayotosheleza ambayo hudumu milele na kutuongoza mbinguni, na njiani kutuweka huru kutoka katika udanganyifu wa dhambi wa utoshelevu mwingine. Anafanya hivi kwa kututumia Roho wake (Yohana 7:38–39).




Comments