top of page

Kwa Nini Hatufi Moyo

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jun 30
  • 2 min read

Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Kwa maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi kupita kiasi, kwa sababu hatuangalii yale yanayoweza kuonekana bali yale yasiyoweza kuonekana. Kwa maana yale yanayoweza kuonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoweza kuonekana ni ya milele. (2 Wakorintho 4:16-18)

 

Paulo haoni jinsi alivyokuwa akiona (na hakukuwa na miwani). Hawezi kusikia jinsi alivyokuwa akisikia (na hakukuwa na visaidizi vya kusikia). Haponi kutokana na vipigo kama alivyozoea (na hakukuwa na dawa za maumivu). Nguvu zake, kutembea kutoka mji hadi mji, haikuwa sawa na jinsi ilivyokuwa zamani. Anaona mikunjo usoni na shingoni. Kumbukumbu yake sio nzuri. Na anakiri kwamba hili ni tishio kwa imani yake na furaha yake na ujasiri wake.

 

Lakini hafi moyo. Kwanini?

Hafi moyo kwa sababu utu wake wa ndani unafanywa upya.

Kivipi?

 

Ufanywaji upya wa moyo wake unatokana na kitu cha ajabu sana: huja kwa kutazama kile asichoweza kukiona.

 

Hatutazamii vitu vinavyoonekana bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda mfupi, lakini visivyoonekana ni vya milele. (2 Wakorintho 4:18)

 

Hii ndiyo njia ya Paulo ya kutokufa moyo: kutazama kile asichokiona. Basi, aliona nini alipotazama?

 

Mistari michache baadaye katika 2 Wakorintho 5:7 , anasema, “Tunaenenda kwa imani, sio kwa kuona.” Hii haimaanishi kwamba anaruka gizani bila ushahidi wa kile kilichopo. Ina maana kwamba kwa sasa mambo halisi ya thamani na muhimu zaidi duniani yapo nje ya milango yetu ya fahamu kimwili.

 

"Tunatazama" vitu hivi visivyoonekana kupitia injili. Tunaimarisha mioyo yetu - tunafanya upya ujasiri wetu - kwa kukaza macho yetu juu ya ukweli usioonekana, ukweli halisi ambao tunauona katika ushuhuda wa wale waliomwona Kristo uso kwa uso.

 

“Mungu, aliyesema, Nuru na iangaze kutoka gizani, ndiye aliyeng’aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo” (2 Wakorintho 4:6). "Nuru ya maarifa wa utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo." Tunaona hili linapoangaza mioyoni mwetu kupitia injili.

 

Tulifanyika kuwa Wakristo wakati hili lilipofanyika - iwapo tunalielewa hili au la. Na pamoja na Paulo tunahitaji kuendelea kuona kwa macho ya moyo, ili tusife moyo.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page