Kwanini Una Mwili
- Dalvin Mwamakula
- Jul 31
- 1 min read

Kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu. (1 Wakorintho 6:20)
Mungu hakuumba ulimwengu wa vitu vya kimwili bila kusudi. Alikuwa na kusudi, yaani, kuongeza namna ambazo utukufu wake unaoneshwa kwa nje na kudhihirishwa. “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na mbingu zaitangaza kazi ya mikono yake” (Zaburi 19:1).
Miili yetu inafaa katika kundi lile lile la vitu vya kimwili ambavyo Mungu aliviumba kwa sababu hii. Hatarudi nyuma katika mpango wake wa kujitukuza kupitia wanadamu na miili ya wanadamu.
Kwanini Mungu anaingia kwenye matatizo yote ili kuchafua mikono yake, yaani, kwenye mwili wetu unaooza, uliotiwa doa na dhambi, ili kuuweka upya kuwa mwili wa ufufuo na kuuvika utukufu na kutokufa? Jibu: Kwa sababu Mwana wake alilipa gharama ya kifo ili kusudi la Baba kwa ulimwengu wa kimwili litimizwe, yaani, kwamba atukuzwe ndani yake, pamoja na miili yetu, milele na milele.
Ndivyo andiko linavyosema: “Mlinunuliwa kwa gharama [yaani, kifo cha Mwana wake]. Basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” Mungu hataweza kupuuza au kudharau kazi ya Mwana wake. Mungu ataheshimu kazi ya Mwana wake kwa kufufua miili yetu kutoka kwa wafu, nasi tutatumia miili yetu kumtukuza milele na milele.
Ndiyo maana unao mwili sasa. Na ndiyo maana utafufuliwa kuwa kama mwili wa utukufu wa Kristo.




Comments