top of page

Kweli Mbili Zenye Nguvu na Upole Usio na Kifani

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 2 min read
ree

". . . nikitangaza mwisho tangu mwanzo na tangu zamani mambo ambayo hayajatendeka, nikisema, ‘Shauri langu litasimama, nami nitatimiza kusudi langu lote." (Isaya 46:10)

 

Neno “Ukuu” (kama neno “Utatu”) halipatikani katika Biblia. Tunatumia neno hilo kurejelea ukweli huu: Mungu yuko katika udhibiti wa mwisho wa dunia kuanzia kwenye njama kubwa za kimataifa hadi kufikia kwa ndege mdogo msituni. 


Hivi ndivyo Biblia inavyosema:


“Mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine. . . . ‘Shauri langu litasimama, nami nitatimiza kusudi langu lote’” (Isaya 46:9–10).


Na: “[Mungu] hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumuuliza, ‘Unafanya nini wewe?’” (Danieli 4:35).


Na: "Yeye habadiliki, na nani anaweza kumrudisha nyuma? Anachotaka, ndicho anachofanya.  Kwa maana atakamilisha kile alichonipangia" (Ayubu 23:13-14).


Na: "Mungu wetu yuko mbinguni; anafanya yote apendayo" (Zaburi 115:3).


Ukuu na rehema ya Mungu ni nguzo zisizoyumbishwa—ni tumaini langu la baadaye, nguvu yangu kwenye huduma, na tiba yangu kwenye kukata tamaa. Na inaweza kuwa yako pia!

Sababu moja ya mafundisho haya kuwa ya thamani kwa waumini ni kwamba tunajua shauku kuu ya Mungu ni kuonyesha rehema na wema kwa wale wanaomwamini (Waefeso 2:7; Zaburi 37:3-7; Mithali 29:25). Ukuu wa Mungu unamaanisha kwamba mpango huu kwetu hauwezi kuvurugwa. Hauwezi kushindwa.


Hakuna kitu, hakuna kabisa, kinachowapata wale “wanaompenda Mungu” na “walioitwa kulingana na kusudi lake” isipokuwa kile kilicho kwa ajili ya mema yetu ya ndani kabisa, ya juu kabisa, na ya muda mrefu zaidi (Warumi 8:28; Zaburi 84:11).


Hii ndiyo sababu napenda kusema kwamba rehema na ukuu wa Mungu ni nguzo mbili za maisha yangu. Ni tumaini la maisha yangu ya baadaye, nguvu ya huduma yangu, kitovu cha theolojia yangu, kifungo cha ndoa yangu, dawa bora katika magonjwa yangu yote, tiba ya kukata tamaa kwangu kote. 


Na nitakapokuja kufa (iwe mapema au baadaye), kweli hizi mbili zitasimama kando ya kitanda changu, na kwa mikono yenye nguvu isiyo na kipimo na yenye upole usio na kipimo zitaninyanyua hadi kwa Mungu.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page